Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

13 Januari 2023

15:15:06
1338090

Mashirika ya kimataifa yaomba kupatiwa bajeti ili kupambana na utapiamlo kwa watoto

Mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yametoa taarifa ya pamoja yakiomba kupatiwa hara bajeti ili kuwasaidia watoto milioni 40 wanaosumbuliwa na utapiamlo mkali.

Shirika la Kimataifa la  Save the Children hivi karibuni lilitangaza kuwa: Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Haiti, Somalia, Sudan Kusini na Yemen ni nchi ambazo zina waathirika wengi wa janga la utapiamlo mkali na wanaohitaji msaada wa dharura. Limesema, kiwango kikubwa cha njaa kimeripotiwa miongoni mwa waathirika hao ikiwa ni kutoka watu milioni mbili na laki tano mwaka 2019 na kufikia milioni sita na laki sita mwaka uliopita wa 2022.   

Mashirika hayo yenye mfungamano na Umoja wa Mataifa yametangaza kuwa, mapigano, taathira za mabadiliko ya tabia nchi, maambukizi ya Uviko-19 na kuongezeka gharama za maisha na mfumuko wa bei za bidhaa yote hayo yamesababisha watoto wengi kukumbwa na utapiamlo. 

Yameongeza kuwa, hivi sasa watoto zaidi ya milioni 30 katika nchi 15 duniani wana utapiamlo mkali; na milioni 8 kati ya watoto hao wana uzito mdogo kulinganishwa na vimo na umri wao.  Nchi hizo ni Afghanistan, Burkina Faso, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Haiti, Kenya, Madagascar, Mali, Niger, Nigeria, Somalia, Sudan Kusin, Sudan na Yemen.  

Janga la utapiamlo kwa watoto wa Sudan Kusini 

Katika upande mwingine, mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yamesisitiza kuwa kuongezeka bei ya bidhaa za chakula kumesababisha kupungua kwa chakula cha mahitajio; ambapo watu wanalazimika kuhama makazi yao na kuelekea sehemu nyingine ili kujidhaminia mahitaji ya chakula cha bei nafuu. 

342/