Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

13 Januari 2023

15:15:32
1338091

Uingereza ni nchi ghali zaidi ya Ulaya kuishi

Takwimu zinaonyesha kuwa Uingereza ndiyo nchi ghali zaidi yabarani Ulaya kuishi kutokana na matatizo makubwa ya kiuchumi na kifedha yanayoikabili nchi hiyo.

Imeelezwa kuwa, ongezeko kubwa la mfumuko wa bei kuwahi kushuhuhudiwa huko Uingreza na ongezeko lisilozuilika la gharama za maisha nchini humo zimeiweka nchi hii katika hali mbaya zaidi ya kiuchumi katika nusu karne iliyopita. 

Utafiti uliofanywa nchini Uingereza, Ujerumani, Uhispania, Ufaransa, Ureno, Ugiriki na Italia unaonyesha kuwa bei ya chakula, pamoja na bei isiyodhibitiwa ya mafuta, tikiti za treni na vitu vingine muhimu ni ghali zaidi nchini Uingereza kuliko katika nchi zingine za Ulaya. 

Aidha imebainika kuwa, gharama kubwa za maisha pia  zimekuwa zikiibua mashinikizo makubwa kwa wastaafu nchini humo. Nchi zote za Ulaya ziko kwenye mtikisiko wa kiuchumi huku  mfumuko wa bei ukiongezeka bila kudhibitiwa, lakini kwa mujibu wa tathmini ya Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), uchumi wa Uingereza uko katika hali mbaya zaidi katika nyanja zote ikilinganishwa na nchi nyingine za G7.   

Matatizo ya kiuchumi na kimaisha nchini Uingereza ni makubwa kiasi kwamba mamia ya maelfu ya watu waajira wa  sekta ya umma, kuanzia wafanyakazi wa reli na posta hadi wauguzi na madereva wa magari ya wagonjwa, waligoma katika siku za mwisho za mwaka jana wa 2022 kupinga hali ngumu ya sasa.Huo unatajw akuwa mgomo mkubwa zaidi wa wafanyakazi wa sekta ya umma nchini Uingereza kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 3o ya karibuni. 

342/