Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

27 Januari 2023

15:09:56
1341426

Moscow: Njama za kuisheheneza silaha Ukraine zimefeli

Serikali ya Russia imesema kuwa, njama za Marekani za kuipa Ukraine vifaru vyake vya Abrams ni fikra iliyofeli na haitosaidia chochote zaidi ya kuitia hasara zaidi tu Ukraine.

Hayo yalisemwa jana (Jumatano) na msemaji wa Ikulu ya Russia, Dmitry Peskov ambaye aliongeza kuwa, kuipa Ukraine vifaru vya Abrams vya Marekani ni fikra iliyoshindwa na kwamba vifaru hivyo kama zilivyo silaha nyingine za Wamagharibi huko Ukraine, vyote vitateketea kwenye moto. 

Amesema, hali barani Ulaya na duniani kiujumla ni tete mno hivi sasa na hakuna faida yoyote inayopatikana katika kuchochea moto wa vita. Vile vile amesema, hakuna fikra wala juhudi zozote za kupunguza mivutano iliyopo kuhusu Ukraine. 

Ukraine imegeuzwa uwanja wa kujaribishia silaha za Magharibi ambazo hata hivyo zinateketea kwa moto

 

Msemaji huyo wa Ikulu ya Russia vile vile amesema, hakuna mazungumzo yoyote yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni baina ya Russia na Ujerumani ya kuishawishi Berlin isipeleke vifaru vyake nchini Ukraine. Amesema, inabidi tuwe macho na tuishi kwa tahadhari kubwa, kwani hakuna matumaini yoyote ya kupungua wasiwasi na mivutano kimataifa kutokana na njia inayofuatwa na jeshi la nchi za Magharibi NATO hivi sasa. 

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimetangaza kuwa nchi hiyo imeamua kuipa Ukraine vifaru vyake vya Leopard 2. Taarifa hiyo imesema pia kuwa, Marekani nayo imekusudia kuipa Ukraine vifaru vyake vya Abrams ili kuipiga vita Russia.

Kwa upande wake serikali ya Moscow imeonya kwamba uamuzi huo wa kuisheheneza silaha Ukraine utajibiwa vikali na Russia na kwamba Moscow nayo itatumia silaha kali zaidi za kukabiliana na silaha hizo za Magharibi.

342/