Main Title

source : Parstoday
Jumapili

29 Januari 2023

18:24:03
1342079

Medvedev atahadharisha kuhusu kutokea Vita vya Tatu vya Dunia

Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Russia amesisitiza kuwa, kitendo cha kuipatia Kiev magari ya kivita na silaha zingine hakutazuia kuibuka Vita vya Tatu vya Dunia.

Serikali ya Ujerumani hatimaye imesalimu amri mbele ya mashinikizo ya waitifaki wake ikiwemo Marekani na kukubali kutuma Ukraine vifaru aina ya Leopard 2. Jarida la Politico pia tarehe 26 mwezi huu liliripoti kuwa, Marekani ina mpango wa kutuma Ukraine vifaru vya sasa zaidi vya Abrams. Dmitry Medvedev Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Russia jana alieleza kuwa, hatua yoyote ya kuiunga mkono na kuipatia misaada ya silaha na zana za kijeshi Ukraine haitakuwa kwa maslahi ya yoyote barani Ulaya. Amesema, kuipatia Ukraine vifaru hivyo tajwa hakutainusuru Ulaya na Vita vya Tatu vya Dunia iwapo vitatokea.  

Medvedev ameongeza kuwa, kwa bahati mbaya kama Vita vya Tatu vya Dunia vitaanza havitapiganwa kwa kutumia vifaru na wapiganaji kwa sababu na hivyo dunia nzima itadhurika. Medvedev amekosoa hatua ya nchi za Magharibi ya kutuma Ukraine silaha na zana nyingi za kivita kwa aiili ya kukabiliana na Russia na kueleza kuwa baadhi ya Mawaziri wa Ulinzi akiwemo Waziri wa Ulinzi wa Italia wanafikiria kutuma magari ya kivita na silaha nyingine huko Ukraine kama njia eti ya kuzuia kuibuka Vita vya Tatu vya Dunia. 

Wakati huo huo, Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Russia amewakosoa viongozi wa Uingereza ambao wanasisitiza kuwa kuna ulazima wa kutumwa haraka misaada ya kijeshi ya nchi wanachama wa Nato huko UKraine na akasema: ndege za kivita, mamia ya vifaru na mifumo ya makombora ya masafa marefu huwenda hiyo ikawa njiaa  njia pekee ya kuzuia upanuzi wa Russia lakini bado itasababisha kutokea Vita vya Dunia. 

342/