Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Tasnim, Luteni Jenerali Robert Peter Bauer, amesema hayo na kuonesha imani yake kwa NATO kuwa iko tayari kuingia vitani moja kwa moja na Russia na kukiri kwamba NATO imepoteza heshima yake ya kuwa mwamuzi mkuu wa masuala ya kijeshi.
Ikumbukwe kuwa sisitizo la rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy la kupewa nchi hiyo makombora ya balestiki ya kupiga ardhi za Russia, upinzani wa nchi za Amerika ya Kusini wa kupelekewa silaha Kiev, uwezekano wa kubadilishwa mkakati wa Washington katika suala zima la kuipaa silaha Kiev, na mahitaji makubwa ya jeshi la Ukraine la ndege 180 za kivita, ni kati ya matukio muhimu zaidi yanayozunguka kadhia ya Ukraine hivi sasa.
Jeshi la Nchi za Magharibi NATO mara kwa mara linadai kuwa halitaki kuingia vitani moja kwa moja na Russia, lakini ukweli ni kwamba kushiriki kwao kikamilifu katika vita vya nchini Ukraine dhidi ya Moscow ni sawa na kuingia vitani moja kwa moja na Russia.
Sasa hivi, Mkuu wa Kamati ya Kijeshi ya NATO amesema, jeshi hilo la nchi za Magharibi liko tayari kwa makabiliano ya moja kwa moja na Russia.
Siku chache zilizopita mkuu wa majeshi ya Russia, Jenerali Valery Gerasimov, aliitaja tamaa ya NATO ya kujitanua kwa kuziongeza Uswisi na Finland kwenye muungano huo na pia kitendo cha nchi za Magharibi cha kuitumia Ukraine kama chombo rahisi cha kuendesha vita kwa niaba ya NATO ndilo tishia kubwa kwa usalama wa kitaifa wa Shirikisho la Russia.
342/