Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

3 Februari 2023

12:42:17
1343306

Sababu za kuongezeka hukumu za kifo nchini Saudi Arabia baada ya Bin Salman kuingia madarakani

Shirika la Haki za Binadamu la Ulaya-Saudia, limetangaza katika ripoti ya karibuni kwamba hukumu za kifo au unyongaji wakati wa utawala wa mrithi wa kiti cha ufalme Mohammed bin Salman nchini Saudi Arabia zinaongezeka karibu mara mbili kila mwaka.

Shirika hilo limesema wastani wa idadi ya watu walionyongwa wakati wa utawala wa Bin Salman na baba yake umeongezeka kwa asilimia 82. Kulingana na ripoti hii, mnamo 2022, Saudi Arabia iliwanyonga watu 147, idadi ambayo ni zaidi ya jumla ya idadi ya hukumu zilizotolewa miaka miwili iliyopita, ambayo ilikuwa kesi 81. Kati ya watu hao 147, watu 81 walinyongwa kwa umati siku moja katika mwezi wa Machi 2022, ambayo ilionekana kuwa idadi kubwa zaidi katika historia ya Saudi Arabia na kufuatiwa na lawama kali za kimataifa.

Aidha kwa mujibu wa ripoti hii, katika miaka ya 2021 na 2022, hukumu zilizotekelezwa ziliongezeka kwa asilimia 119, na utoaji wa hukumu hizo uliongezeka kwa asilimia 444 katika miaka ya 2020 hadi 2022. Kulingana na kituo hicho rasmi cha haki za binadamu, hukumu za kifo 27 zilitekelezwa mnamo 2020 na 67 mnamo 2021.

Kwa mujibu wa muundo wa kijadi na kimadhehebu wa Ufalme Saudi Arabia, unyongaji ni jambo ambalo limekuwepo tangu mwanzo wa kuundwa kwa ufalme huo, lakini kwanza, idadi ya watu walionyongwa haikuwa kubwa sana, na pili, kunyongwa huko kulizingatia hukumu za kimadhehebu kabla ya Bin Salman kunyakua madaraka.

Punde baada Bin Salman kinyakua madaraka, sheria za kidini hazikuzingatiwa tena kwani amekandamiza na kudhoofisha kabisa misingi ya kidini katika mfumo wa kisiasa wa Saudia ambapo ufalme huo sasa umechukua muelekeo wa kisekula. Kwa msingi huo unyongaji wafungwa sasa unazingatia zaidi misimamo ya kisiasa ambapo wengi walionyongwa ama ni wakosoaji wa Bin Salman au wale waliopinga kuharibiwa kwa nyumba zao kwa ajili ya kupisha mradi mkubwa wa mabilioni ya dola wa mji wa kisasa wa Neom. Hivyo kimsingi wanaonyongwa Saudia hivi sasa ni wale wanaomkasirisha Bin Salman.

Jambo muhimu na la kuzingatia katika muktadha huu ni kwamba nchi za Magharibi kwa kawaida hupinga hukumu za kifo ambazo zina muelekeo wa kidini, lakini sasa kwa kuwa hukumu nyingi za kunyongwa Saudia zina muelekeo wa kisiasa na zinatumiwa na Bin Salman kunyamazisha wapinzani, nchi za Magharibi zimeamua kunyamaza kimwa. Hivyo nchi hizo hazijali masuala ya haki za inaadamu maadamu Bin Salman ni muitifaki wao.

Kwa kuzingatia hilo, inaweza kusemwa kuwa, moja ya sababu za kuongezeka hukumu za kunyongwa nchini Saudi Arabia baada ya bin Salman kuingia madarakani ni kutokana na misimamo ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi na mashirika ya kimataifa. Kile ambacho nchi za Magharibi na mashirika ya kimataifa yanafanya ni hatua ya kimaonyesho ya kutoa taarifa dhaifu kabla ya kutekelezwa hukumu za kunyongwa Saudia.

Nukta nyingine ya kuzingatiwa ni hii kwamba, kuna uhusiano mkubwa kati ya kurejeshwa uhusiano kati ya Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongezeka idadi ya wanaonyongwa Saudia katika zama za Bin Salman.

Nukta hii inaonesha kuwa Bin Salman anatumia umafia wa Kiyahudi na ushawishi katika nchi za Magharibi kama njia ya kuimarisha misingi yake ya utawala kwa kuwanyonga wapinzani.

Hakuna shaka kuwa utawala wa Kizayuni unapinga demokrasia katika nchi za Kiarabu na unapendelea udikteta kuliko demokrasia katika nchi hizo kutokana na kuwa aghalabu ya wananchi wanapinga uhusiano na utawala huo na hivyo iwapo uchaguzi huru utafanyika, utawala kama ule wa Saudia utaondolewa madarakani mara moja.

Wananchi wa nchi za Kiarabu walibainisha bayana upinzani wao kwa uhusiano na Israel wakati wa michezo ya Kombe la Dunia la Doha.

Katika upande mwingine hivi sasa utawala wa Kizayuni wa Israel unakumbwa na mgogoro mkubwa kwani wapinzani wa waziri mkuu Netanyahu wanasema kwamba ameiondoa Israeli kwenye mkondo wa 'demokrasia' na sasa utawala huo unaelekea katika udikteta kamili.

342/