Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

4 Februari 2023

11:35:31
1343516

Iran: Wakiukaji wa kila siku wa haki za binadamu ni wabeba bendera ya uongo ya haki za binadamu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, watu ambao ndio wakiukajii wakubwa wa kila siku wa haki za binadamu ulimwenguni, leo ni wabeba bendera ya uongo ya kutetea haki za binadamu.

Nasser Kan'ani Chafi ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwamba: Waitifaki wa kimkakati wa Marekanii na washirika wa Ulaya katika eneo la Asia Magharibini tawala ambazo kwa mujibu wa takkwimu za Wizara ya Afya ya Palestina mwaka uliopita wa 2022 ziliwaua Wapalestina 277 wakiwemo watoto wadogo 53.

Kan'ani Chafi ameongeza kuwa, mbali na mauaji hayo, Wapalestina wengine 10,500 walijeruhiwa huku wafanyakazi wa mashiriika ya misaada ya kibinadamu na magari yao ya kubebea wagonjwa yakilenga na makombora.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, wale ambao ndio wakiukaji wakubwa wa kila siku wa haki za binadamu wanajifanya kuwa ni watetezi wa haki za binadamu. 

Katika ujumbe wake mwingine wa twitter, Nasser Kan'ani Chafi ameandika, mwezi uliopita wa Januari Wapalestina 35 waliuawa shahidi na utawala haramu wa Israel katika mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, ambapo huo ni mtazamo mwingine wa himaya na uungaji mkono wa madola ya Magharibi kwa suala la haki za binadamu.

Matamshi ya Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni ukweli mchungu ambao umekuwa ukishuhudiwa ulimwengu hivi sasa kwa miaka kadhaa ambapo madola makubwa ya dunia hasa yanayouunga mkono utawala dhalimu wa Israel yamekuwa na undumakuwili na unafiki kuhusiana na suala la hakki za binadamu.

342/