Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

4 Februari 2023

11:37:51
1343521

Palestina yafichua: Ulaya inatushinikiza tuchukue msimamo wa kuilaani Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amefichua kuwa Ulaya inaishinikiza Palestina ichukue msimamo wa kuilaani Russia sambamba na kueleza kwamba amepokea mwaliko kutoka kwa mwenzake wa Russia wa kuzuru Moscow.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la Sputnik, Riyadh Al-Maliki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, ametangaza kuwa, katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, amealikwa na mwenzake huyo wa Russia kuitembelea Moscow.

Al-Maliki amesema, siku zote huwa anafurahi kukutana na Lavrov ili kubadilishana mawazo na kuzungumza kuhusu masuala ya pande mbili, kikanda na kimataifa, na akaongezea kwa kusema: "tutaangalia ni lini ziara hii itafanyika. Ninafikiria kusafiri kwenda Moscow kukutana na Sergey Lavrov labda katika miezi miwili ijayo".
Katika sehemu nyingine ya maelezo yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amefichua kuwa: nchi za Ulaya zinajaribu kutoa mashinikizo dhidi ya Palestina kuitaka ichukue msimamo wa kuilaani Russia kwa hatua yake ya kuivamia kijeshi Ukraine.../


342/