Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

4 Februari 2023

11:38:41
1343524

Waislamu waadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa Imam Ali bin Abi Twalib (AS)

Iran imejiunga na uliwengu wa Kiislamu hii leo katika kuadhimisha siku ya kukumbuka kuzaliwa Amirul Muumin Ali (A.S) Imam wa Kwanza wa Waislamu wa Kishia ulimwenguni.

Wananchi waislamu wa Iran wanaadhimisha siku hii ya kumbukumbu ya kuzualiwa Imam Ali bin Abi Twalib (AS) kwa sherehe mbalimbali kwa kukusanyika katika maeneo matukufu, misikitini na kumbi za masuala ya kijamii. 

Aidha maelfu kwa maelfu ya mazuwwar hapo jana walikusanyika katika Haram tukufu ya Imam Ali (AS), katika mji mtakatifu wa Najaf, Iraq kwa ajili ya maadhimisho hayo.

Siku kama ya leo miaka 1467 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, alizaliwa katika nyumba tukufu ya al Kaaba, Ali bin Abi Twalib (AS), ambaye ni binamu, mkwe na Khalifa wa Mtume Muhammad (saw).

Ali bin Abi Twalib (AS) alizaliwa katika nyumba tukufu ya al Kaaba tarehe 13 Rajab miaka 23 kabla ya Hijra ya Mtume (SAW) kuelekea Madina na katika nyakati za utotoni alilelewa na kupata elimu na mafunzo kutoka kwa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW).

Alikuwa mwanaume wa kwanza kuukubali Uislamu; na alikuwa msaidizi mkuu wa Mtume  Mtukufu (S.A.W) katika marhala zote za tablighi na kueneza mafunzo ya dini ya Uislamu za Mtume wa Uislamu. 

Katika Kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Imam wa Kwanza wa Waislamu Ulimwenguni imepewa jina la "Siku ya Baba." 

Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran linatoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu na wapigania ukombozi wote duniani kwa mnasaba huu wa kukumbuka kuzaliwa Amirul Muuminin Ali (AS), ambaye aliuawa shahidi kwa kupigwa upanga akiwa katika ibada ya Swala ndani ya Msikiti wa Kufa nchini Iraq. 

342/