Main Title

source : ParstodayParstoday
Ijumaa

17 Novemba 2023

19:39:03
1412506

Afrika Kusini yaipeleka Israel kwenye mahakama ya ICC kuhusu mashambulizi ya Gaza,Bunge lajadili kukata uhusiano

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake imewasilisha ombi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kwa ajili ya kutaka uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita unaoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel huko Gaza huku bunge likijadili uwezekano wa kukata uhusiano na Israel.

Hatua hiyo inajiri huku wabunge wa Afrika Kusini  wakijadili pendekezo la kuufunga ubalozi wa utawala wa Kizayuni Israel  sambamba  na kukatwa uhusiano wote wa kidiplomasia na Israel hadi itakapokubali kusitishwa kwa mapigano. Mwenyektii wa chama cha EFF Julius Malema aliyewasilisha muswada huo alisema Afrika Kusini haiwezi kuwa na uhusiano na utawala ambao unawaua watoto na wanawake.

Akizungumza akiwa safarini Qatar, Rais Ramaphosa alisema nchi yake inaamini kuwa Israel inafanya uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari huko Gaza, ambako maelfu ya Wapalestina wameuawa katika hujuma ya utawala haramu wa Israel tangu Oktoba 7 na hospitali na miundombinu ya umma pia imeharibiwa.

Ramaphosa  alisema  Afrika Kusini inashirikiana na nyingine nyingi duniani katika kuishtaki Israel kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.Aliongeza kuwa kesi hiyo imewasilishwa kwa sababu utawala Israel unatenda jinai za kivita katika eneo la Gaza ambalo liko chini ya mzingiro wa utawala huo. Hivi karibuni Afrika Kusini ilitangaza kuwarejesha nyumbani wanadiplomasia wake wote kutoka Tel Aviv. Uamuzi huo ulichukuliwa kutokana na kuendelea mashambulizi na jinai za Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina. Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi kubwa na zenye ushawishi barani Afrika, na ndiyo inayoongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi duniani. Raia wengi wa Afrika Kusini wamepitia adha na manyanyaso ya ubaguzi wa rangi kwa miaka mingi. Chama tawala cha African National Congress (ANC), ambacho kina idadi kubwa zaidi ya wabunge katika bunge la kitaifa lenye viti 400, kilisema kitaunga mkono hoja ya EFF ya kufunga ubalozi wa utawala wa Israel na kukata uhusiano wa kidiplomasia na utawala huo hadi ukubali kusitisha mauaji ya kimbari Gaza.


342/