Akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi katika mji mkuu Kinshasa, Moïse Katumbi ameahidi 'kuikomboa nchi' siku ya uchaguzi wa Kongo.
Moïse Katumbi ameahidi kuikomboa nchi hiyo kwa kutoa ajira kwa vijana na kushusha thamani dola ya Marekani mkabala wa sarafu ya nchi hiyo.
“Nimekuja kubadilisha nchi, nimekuja kuikomboa nchi wana Kongo, tutakomboa nchi kwa pamoja", amesisitiza mpinzani huyo mkubwa wa Rais Félix Antoine Tshisekedi ambaye wapinzani wake wameibua swali kuhusu uraia wake, katika kilele cha malumbano yaliyoibuliwa katikati ya wiki na Waziri wa Ulinzi na mbabe wa zamani wa kivita Jean-Pierre Bemba, ambaye alidai kuwa Moïse Katumbi ni Mzambia."Wanasema mimi ni raia wa kigeni, lakini wageni ni wale ambao wamefanya zaidi ya safari 666 nje ya nchi", amesisitiza Katumbi mbele ya hadhara ya maelfu ya mashabiki wake mjini Kinshasa. Mfanyabiashara tajiri na mmiliki wa klabu maarufu ya soka ya TP Mazembe, Moïse Katumbi ni gavana wa zamani (2007-2015) wa jimbo lenye utajiri wa madini la Katanga, lenye nguvu kubwa ya kiuchumi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
342/