Main Title

source : Parstoday
Jumanne

30 Januari 2024

19:42:01
1433823

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu abainisha wajibu wa serikali na sekta binafsi katika maendeleo ya kiuchumi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja himaya ya serikali hususan kuondoa vizuizi katika anga ya biashara na shughuli za sekta binafsi kuwa ni mambo mawili muhimu na yanayoandaa mazingira bora na kupatikana maendeleo makubwa ya nchi.

Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo Jumanne alipokutana na kuzungumza na wanaharakati wa uchumi na wazalishaji wa sekta mbalimbali. Ameashiria suhula na uwezo wenye taathira kubwa wa sekta binafsi kwa ajili ya kutimiza malengo makubwa ya kiuchumi na kuitaka serikali ifuatilie kwa jadi maombi yote yaliyowalishwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha maeneo mengi ya viwanda, kuyafadhili kifedha makampuni ya kati na madogo na kushughulikia suala la kilimo cha kisasa cha umwagiliaji. Ayatullah Khamenei ameashiria masuala yanayokwamisha mipango ya maendeleo kama vile vikwazo na kuwajibika kwa kiwango cha chini kwa kwa baadhi ya serikali zilizotangulia na kusema: Juhudi na maendeleo ya sekta ya kibinafsi, licha ya vikwazo hivyo, yanatoa matumaini kwamba sekta hii inaweza kuifikisha Iran kwenye ustawi unaohitajika wa Mpango wa 7 wa miaka mitano, yaani ukuaji wa asilimia 8 wa uchumi. Ayatullah Khamenei ametaja himaya ya serikali katika nchi mbalimbali duniani kwa mashirika na makampuni yao makubwa kuwa ni moja ya sababu za mafanikio ya makampuni hayo na akasema: Moja ya misaada muhimu ya serikali kwa sekta binafsi ni kusaidia ustawi wa mauzo ya nje na kupata masoko ya ng'ambo, na katika uwanja huu Serikali pamoja na sekta binafsi zinapaswa kushirikiana katika kuimarisha diplomasia ya uchumi. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei ameashiria umatatizo yanayosababishwa na nchi ajinabi kama vikwazo na uhasama wa mabeberu na kusema: Mambo haya bila shaka yanatoa pigo na kuisababishia nchi matatizo, lakini masuala haya yanaweza pia kuandaa fursa, kama ambavyo vijana wetu walivyotumia vyema na fursa hizo; na leo hii wamefanikiwa kuunda silaha za kisasa za kijeshi na kupata mafanikio ya kisayansi kama hatua za maendeleo zinazoshuhudiwa katika sekta ya anga za mbali. 

342/