Main Title

source : Parstoday
Jumatano

31 Januari 2024

20:08:07
1434115

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu azuru Haram ya Imam Khomeini (MA) na makaburi ya Mashahidi

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amezuru Haram tukufu ya Imam Khomeini (MA) na makaburi ya Mashahidi ya Behesht Zahraa sambamba na kuanza maadhimisho ya Alfajiri Kumi za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa kitengo cha habari cha Ofisi ya Kiongozi Muadhamu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezuru haram tukufu ya Imam Khomeini (MA) na kaburi la mwana na kumbukumbu ya mwasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuwapigia faatiha.Ayatullah Khamenei amezuru pia makaburi ya Mashahidi 72 wa tukio la kigaidi la tarehe 7 Tir na Mashahidi wa mripuko uliotokea ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 1980 na kuenzi kumbukumbu za Mashahidi Beheshti, Rajaei, Bahonar na wenzao waliouawa shahidi pamoja nao.Vilevile Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezuru makaburi ya Mashahidi adhimu wa Mapinduzi ya Kiislamu, wa vita vya miaka minane vya Kujihami Kutakatifu na wa ulinzi wa Haram tukufu ya Bibi Zainab (SA).Miongoni mwa makaburi ya Mashahidi ambayo Ayatullah Khamenei ameyazuru ni la Shahidi Mohammad Amin Samadi ambaye aliuawa shahidi hivi karibuni katika shambulio la kigaidi lililofanywa na utawala wa Kizayuni katika mji mkuu wa Syria, Damascus.../

342/