Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

3 Februari 2024

19:35:47
1434893

Raisi: Jibu la Iran kwa shambulio lolote tarajiwa litakuwa kali

Rais Ebrahim Raisi wa Iran anasema Iran haitoanzisha vita lakini itatoa jibu kali na lenye nguvu kwa chokochoko ya aina yoyote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Raisi ameyasema hayo katika hotuba yake kwa umati mkubwa wa watu Ijumaa katika mji wa Minab katika jimbo la Hormozgan kusini mwa Iran. Rais wa Iran ameongeza kuwa: "Tumesema mara nyingi kwamba hatutakuwa waanzilishi wa vita vyovyote, lakini ikiwa nchi au jeshi la kikatili litataka kuidhulumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, basi jibu letu litakuwa kali."

Amesema nguvu za kijeshi za Iran si lolote kwa nchi za Asia Magharibi bali ni chanzo cha usalama ambacho mataifa ya eneo hilo yanaweza kutegemea.

Raisi alisema maadui walikuwa wakitumia lugha ya vitisho dhidi ya Iran na hata kusema chaguo la kijeshi liko mezani, lakini sasa wanatangaza kwamba hawataki makabiliano yoyote ya kijeshi na Jamhuri ya Kiislamu.

Raisi alisisitiza kuwa uwezo wa kijeshi wa Iran una lengo la kujihami na kumzuia adui.

Rais wa Iran ameashiria maonyesho ya Jeshi la Walinzi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambayo ameyatembelea mapema jana asubuhi na kusema maadui hawawezi kuvumilia uvumbuzi unaofanywa na wataalamu wa Iran.Maafisa wa Marekani katika siku za hivi karibuni wamezungumza kuhusu mipango ya kuanzisha mfululizo wa mashambulizi dhidi ya maslahi ya Iran ndani ya Iraq na Syria ili kukabiliana na shambulio lililowaua wanajeshi watatu wa Marekani huko Jordan wiki iliyopita. Rais wa Marekani Joe Biden alilaumu kile alichokiita "makundi yanayoungwa mkono na Iran" hasa yenye makao nchini Iraq kwa shambulio hilo, ambalo pia lilijeruhi takriban askari 34.

Iran imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na mashambulizi dhidi ya vikosi vya Marekani katika eneo, na kusema makundi ya muqawama katika hayachukui amri kutoka Tehran, wala Jamhuri ya Kiislamu haina nafasi katika maamuzi yao ya kutekeleza operesheni za kulipiza kisasi katika kuwalinda wananchi wa Palestina.


342/