Main Title

source : Parstoday
Jumapili

4 Februari 2024

18:19:32
1435178

Hizbullah: Iran inaunga mkono muqawama pasi na kutaraji kitu mkabala wake

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesifu uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa harakati za muqawama na kusema kuwa, uungaji mkono huo unafanyika bila ya kutarajia kitu chochote mkabala wake.

Sheikh Naim Qassim ameeleza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mkono wa urafiki kwa nchi za eneo na harakati za kupigania uhuru za kieneo ili kukabiliana na mfumo wa kibebeberu na uvamizi.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, ingawa Iran inaunga mkono Hizbullah, makundi ya muqawama ya Palestina na harakati nyinginezo za muqawama katika eneo, lakini haiingilii masuala ya ndani ya nchi za eneo.

Sheikh Naim Qassim ameashiria operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba na baadaye vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na kusisitiza kwamba, utawala haramu wa Israel umeshindwa kufikia malengo yake katika hujuma hiyo ya kinyama dhidi ya ngome ya muqawama huko Palestina.Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesifu uungaji mkono amesikitishwa na ukweli kwamba, baadhi wanaikosoa Hizbullah kwa kuunga mkono Gaza, akisema nchi zote za Kiislamu na Kiarabu zinapaswa kufanya hivyo. Kadhalika ameeleza kwamba, ana matumaini muqawama wa Palestina utaibuka na ushindi na hivyo kumzuia adui Mzayuni asifike malengo yake haramu huko Palestina.

342/