Main Title

source : Parstoday
Jumapili

4 Februari 2024

18:20:05
1435179

Ebrahim Raisi: Mapinduzi ya Kiislamu daima yanatilia mkazo elimu na maarifa

Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran muda wote imekuwa ikitilia mkazo elimu na maarifa na kwamba, mara kwa mara Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anahimiza wajibu wa kuimarishwa na kutiiwa nguvu mashirika yenye msiingi wa elimu katika maisha ya wanadamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Sayyid Ebrahim Raisi amesema hayo leo asubuhi kwenye sherehe za kuwaenzi wasomi wa Iran waliopata medali katika mashindano ya kielimu duniani na kusisitiza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu muda wote yanatilia mkazo elimu, kujiimarisha kisayansi, kuongeza maarifa na kunyanyua viwango vya kunufaika na teknolojia za kisasa.

Ameongeza kuwa, hivi sasa Iran ina zaidi ya wahadhiri laki moja wa vyuo vikuu wakati kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaani mwaka 1978 idadi ya wahadhiri na idadi ya vyuo vikuu humu nchini ilikuwa chache sana. Hivi sasa Iran imefikisha makala 78,000 za kielimu wakati kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaani mwaka 1978 ilikuwa na makala 500 tu za kielimu.Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, kuna wajibu wa kuhakikisha kwamba, athari za mafanikio hayo makubwa ya kielimu zionekane waziwazi kwenye maisha ya kawaida ya wananchi hasa kwa kuzingatia kuwa vijana wa Iran wana vipaji vya kila namna kwenye uwanja huo. Amesema, ni jambo lisilo na shaka kwamba hadhi na daraja ya kielimu ya Iran hivi sasa ni kubwa, lakini hiyo haitoshi na hatupaswi kujipweteka, bali ni wajibu kwetu kufanya jitihada kubwa zaidi za kujiimarisha kwa elimu, sayansi na teknolojia za kisasa. Vile vile amesema sekta ya uvumbuzi na ubunifu ni muhiimu mno na ni wajibu kwa taifa kuwa na fikra, ubunifu na nadharia mpya katika kila kona.

342/