Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

12 Februari 2024

19:22:17
1437175

Jeshi la Yemen latekeleza operesheni nyingine dhidi ya meli ya Marekani katika Bahari Nyekundu

Msemaji wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vimetekeleza operesheni nyingine dhidi ya meli ya Marekani katika Bahari Nyekundu.

Brigedia Jenerali Yahya Saree, ametangaza leo kuwa, Jeshi la wanamaji la nchi hiyo limeilenga meli ya Marekani iitwayo Star Iris kwa makombora kadhaa.

Saree ameongezea kwa kusema: "vikosi vya ulinzi  vya nchi hii vitaendelea kutekeleza uamuzi wao wa kuzuia safari za meli zinazoelekea bandari za utawala wa Kizayuni huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu hadi zitakapokomeshwa hujuma na kuondolewa mzingiro iliowekewa Gaza na utawala wa Kizayuni".

Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen ameendelea kusisitiza kuwa: vikosi vya Yemen havitasita kutekeleza operesheni zaidi za mashambulio katika kujibu jinai zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza na vilevile kujibu hujuma za Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen.

Shirika la Operesheni za Biashara ya Baharini la Uingereza limetangaza katika taarifa mapema leo asubuhi kwamba limepokea ripoti ya kujiri tukio la kiusalama kilomita 40 kusini mwa bandari ya al-Mukha ya Yemen.Katika wiki za hivi karibuni, na katika kuunga mkono Muqawama wa taifa la Palestina katika Ukanda wa Gaza, jeshi la Yemen limezilenga katika eneo la Bahari Nyekundu na Mlango-Bahari wa Bab al-Mandab meli kadhaa za utawala wa Kizayuni au zinazoelekea bandari za utawala huo katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Vikosi vya jeshi la Yemen vimeahidi kuwa vitaendelea kushambulia meli za Israel au zile zinazoelekea kwenye bandari zake huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu hadi utawala huo wa Kizayuni utakaposimamisha mashambulio yake dhidi ya Gaza. Wakati huohuo, vikosi vya jeshi la Yemen vimesisitiza na kutamka bayana kuwa, meli nyingine zote ziko huru na zitakuwa na usalama kamili wa kufanya safari zao za baharini katika Ghuba ya Aden na Bahari Nyekundu. Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, kwa uungaji mkono kamili wa Marekani, utawala ghasibu wa Kizayuni umeanzisha mashambulio ya kinyama na mauaji makubwa ya kimbari katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu madhulumu na wasio na ulinzi wa Palestina, na kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu mbele ya jinai hizo za Israel kimepelekea kuendelezwa mauaji hayo ya wanawake na watoto wa Kipalestina yanayofanywa kupitia moto wa vita uliowashwa na utawala huo haramu.../

342/