Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

17 Februari 2024

18:09:18
1438506

Iran yawakamata magaidi waliohusika na hujuma dhidi ya kituo cha polisi Sistan na Baluchestan

Vikosi vya usalama vya Iran vimewakamata magaidi wawili waliohusika katika shambulizi la kigaidi mwezi Disemba mwaka jana kwenye makao makuu ya polisi ya Kaunti ya Rask katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini mashariki mwa nchi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi la Iran, Brigedia Jenerali Saeed Montazer-al-Mahdi, amesema kuwa watu hao wametambuliwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi linalojiita Jaish al-Adl lenye makao yake Pakistan, ambalo lilidai kuhusika na shambulio hilo. Walikamatwa katika moja ya wilaya za Sistan na Baluchestan kufuatia ufuatiliaji wa askari polisi, aliongeza, bila kutaja tarehe ya kuzuiliwa. Montazer-al-Mahdi amebainisha zaidi kuwa magaidi wengine wanne walikuwa wamezuiliwa kwa muda wa wiki kadhaa zilizopita kwa kuhusika na shambulio hilo hilo. Mwishoni mwa Januari 16, ngome mbili kuu za kundi la kigaidi linalojiita Jaish al-Adl katika mkoa wa kusini-magharibi mwa Pakistan wa Balochistan zilishambuliwa kwa makombora makini na kuangamizwa kabisa katika operesheni maalumu ya vikosi vya usalama vya Iran.Vituo hivyo vililengwa na kubomolewa kwa mafanikio katika eneo la Koh-e-Sabz katika jimbo hilo, ambalo linajulikana kuwa miongoni mwa ngome kuu za magaidi wa Jaish al-Adl. Kundi linalojiita Jaish al-Adl ni kundi la kigaidi la kidhalimu ambalo hutekeleza mauai ya kinyama na lina makao yake makuu nchini Pakistan. Kundi hilo limehusika katika mashambulizi mengi ya kigaidi dhidi ya Iran. Mnamo Desemba 15 mwaka jana, kikundi hicho kilidai kuhusika na shambulio la makao makuu ya polisi ya Kaunti ya Rask.

342/