Main Title

source : Parstoday
Jumapili

18 Februari 2024

15:58:48
1438768

Kiongozi Muadhamu asisitiza mahudhurio katika uchaguzi na kulindwa umoja wa kitaifa

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa umoja wa kitaifa na kuutaja uchaguzi ujao wa tarehe Mosi ya mwezi ujao wa Machi kuwa ni utatuzi wa matatizo na urekebishaji wa mambo na kutoa wito kwa kila mtu kushiriki kwa hamasa katika tukio hilo muhimu la kitaifa.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hayo leo katika kikao chake na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Azerbaijan Mashariki na kuiona kambi ya Uistikbari kuwa inapinga uchaguzi wa Iran na kusema: Uchaguzi ni dhihirisho la mfumo wa jamhuri na ndio maana mabeberu na Marekani, ambao wanapinga mfumo wa jamhuri na Uislamu, wanapinga uchaguzi na mahudhurio ya watu kwa hamasa kwenye vituo vya kupigia kura.

Akizungumzia takwa la mmoja wa marais wa zamani wa Marekani kwa wananchi wa Iran la kutoshiriki katika uchaguzi uliopita amesema: Rais huyo bila kujua aliisaidia Iran kwa sababu wananchi walishiriki kwa hamasa zaidi katika uchaguzi huo ili kuonyesha ukaidi na upinzani dhidi yake, na ndio maana Wamarekani hawazungumzi tena namna hii, lakini wanajaribu kuwaweka watu mbali na uchaguzi kwa kutumia njia tofauti.Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja uchaguzi kuwa nguzo kuu ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na njia ya kurekebisha nchi na kusema: Kila mtu anapaswa kushiriki katika uchaguzi huo; na wanaotafuta marekebisho na kutatua matatizo, njia sahihi ni uchaguzi na waende katika vituo vya kupigia kura na kupiga kura. Ayatullah Khamenei amewaasa watu waliojitosa katika uchaguzi kuwania nyadhifa mbalimbali kwa kuwaambia, wanapaswa kujiepusha na tabia mbaya, matusi, kuvunjiana heshima na tuhuma dhidi ya wengine katika matangazo na mitandao, na pia kuchafua wengine na kueleza mambo ya uongo na yasiyo ya kweli ili kuvutia hisia za watu, kwa sababu vitendo hivyo vitasababisha kuondoka uaminifu.

342/*