Main Title

source : Parstoday
Jumatano

21 Februari 2024

12:48:37
1439468

Eslami: Iran ni miongoni mwa nchi 5 zinazoongoza katika sekta ya nyuklia

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema kuwa nchi hii ni kati ya nchhi tano zinazoongoza duniani katika sekta ya nyuklia licha ya vikwazo vya miaka kadhaa vya Magharibi dhidi ya Tehran.

Mohammad Eslami ameashiria mafanikio ya Iran katika miradi yake ya kuzalisha nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani ikiwemo uzalishaji wa maji mazito ya kiwango cha juu na kusema Iran imeorodheshwa miongoni mwa nchi tano bora duniani katika nyanja nyingi kama vile sekta ya nyuklia.Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ameeleza kuwa: Leo hii Iran ipo katika orodha ya juu kwa upande wa ubora na usafi wa maji mazito ya viwanda vya nishati ya nyuklia yanayozalishwa bila msaada wa nchi za kigeni, bali kupitia utafiti wa wanasayansi wa Kiirani. Mohammad Eslami ameongeza kuwa, maji mazito yanaweza kutumika katika utengenezaji wa miundo na vifaa vidogo sana vya elektroniki (microelectronics) na baadhi ya dawa mpya. Eslami pia amezungumzia vikwazo ilivyowekewa Iran katika njia ya maendeleo ya kisayansi, sekta ya nyuklia na masuala ya anga na kusema: Katika miaka iliyopita, Iran imesajili mafanikio mengi katika miradi yake ya nyuklia mkabala wa vikwazo vya Marekani. Iran pia imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ikiwa nchi iliyosaini Mkataba wa NPT.

342/