Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

3 Mei 2024

14:12:52
1455925

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Niger asisitiza juu ya kuimarisha uhusiano na Iran

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Niger amesisitiza kuhusu kuimarishwa uhusiano baina ya nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi.

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Niger Mallam Seydou Asman, katika mahojiano maalum na Hausa TV ya Kanali ya Sahab, amepongeza juhudi za Iran za kupanua uhusiano na nchi za Kiafrika. Amebainisha matumaini yake kuwa mikataba ambayo imetiwa saini hivi karibuni na maafisa wa nchi mbili inapaswa kutekelezwa haraka iwezekanavyo.

Seydou Asman ameongeza kuwa: Iran leo imekuwa mfano wa kuigwa na nchi yetu yenye kila aina ya utajiri kama vile madini, mafuta ya petroli, vyanzo vya maji, ardhi yenye rotuba, mufugo n.k

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Niger ameashiria kuwa, alichokiona katika safari hii nchini Iran ni kinyume na inavyosemwa kuhusu nchi hii, ambapo maendeleo ya Iran katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kibiashara, kisayansi, kiteknolojia, kiufundi na kiuhandisi ni ya kupongezwa.

Akielezea kufurahishwa kwake na matokeo chanya ya safari yake nchini Iran na mazungumzo na maafisa wakuu wa Iran, Seydou Asman amebainisha kuwa: Safari hii ilifanywa ili kujifunza zaidi kuhusu ustaarabu, utamaduni na maendeleo ya Iran na pia kutangaza azma ya serikali ya Niger ya kuimarisha uhusiano na Iran.

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Niger ameashiria pia juhudi za vyombo vya habari vya Magharibi za kuwasilisha sura potofu kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa: Kinyume na propaganda za Magharibi, Iran ni nchi huru na iliyostawi.

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Niger, Mallam Seydou Asman, alifika Iran na kushiriki katika mkutano wa pili wa kimataifa wa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Iran na Afrika ambao ulihudhuriwa na nchi 30 za Afrika na kufuatiawa na maonyesho ya wiki moja ya kibiashara ya Iran Expo 2024 yaliyomalizika Mei Mosi.

Afrika daima imekuwa moja ya vipaumbele vya siasa za nje za Iran katika kipindi cha baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

342/