Main Title

source : Parstoday
Jumanne

28 Mei 2024

16:47:13
1461893

Ali Bagheri Kani: Uhusiano imara miongoni mwa nchi jirani utapelekea kufurushwa nchi vamizi Asia Magharibi

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa uhusiano imara miongoni mwa nchi jirani za kanda hii ni njia pekee ya kuzifurusha nchi vamizi katika eneo la Asia Magharibi.

Ali Bagheri Kani alieleza haya jana katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Sayyid Badr al Busaidi Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Oman ambaye aliwasili Tehran jana kuwasilisha salamu za rambirambi na kuonyesha mshikamano na Iran kufuatia kufa shahidi Rais Sayyid Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir- Abdollahian katika ajali ya helikopta wiki iliyopita. 

Akizungumza jana na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Oman amesema: "Leo, tunaunganisha uhusiano wa kirafiki na wa kidugu na kukuza uhusiano wa kimataifa na majirani zetu". Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu imedhamiria kwa dhati kuzuia kuibuka mpasuko na hitilafu katika uhusiano wake chanya kati yake na majirani zake.

Ali Bagheri Kani Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na mgeni wake Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Oman wamejadili mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza juu ya haja ya kufanyika juhudi kubwa ili kusitisha jinai za utawala wa Kizayuni na kufanikisha utumaji wa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Gaza walioathiriwa na mauaji ya kimbari. 

342/