Main Title

source : Parstoday
Jumatano

29 Mei 2024

20:52:42
1462127

Katibu Mkuu wa UN: 'Mateso' ya Gaza lazima yakomeshwe baada ya shambulio kubwa la Rafah

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao katika mji wa Rafah, kusini mwa Gaza, akitaka kukomesha mara moja kile ilichokiita hofu na mateso katika maeneo yote ya Wapalestina.

Katika taarifa yake, António Guterres ametoa wito wa kusitishwa hofu na mateso mara moja huko Gaza. Vilevile amesisitiza matakwa yake ya kusitishwa mara moja mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Guterres amekumbusha uamuzi uliotolewa hivi karibuni na mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa iliyoiamuru Israel kusitisha mara moja mashambulizi yake ya nchi kavu huko Rafah.

Amesisitiza kuwa maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ni ya lazima kisheria na Israel inalazimika kuyatekeleza."Mamlaka za Israel lazima ziruhusu na kuwezesha utoaji wa haraka, salama na bila ya kizuizi wa misaada ya kibinadamu kwa wale wanaohitaji, na maeneo yote ya kupita lazima yawe wazi," amesema Katibu Mkuu wa UN katika ujumbe wake uliosomwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stéphane Dujarric.

Mashambulizi ya wiki tatu ya Israeli dhidi ya mji wa Rafah yameibua hasira kote duniani husuan baada ya shambulio la anga Jumapili (Mei 26) katika kambi ya wakimbizi na kuua Wapalestina wasiopungua watu 45.


342/