Main Title

source : Parstoday
Jumatano

29 Mei 2024

20:54:19
1462129

Kuendelea maandamano dhidi ya Israel nchini Uturuki

Maandamano ya wananchi wa Uturuki ya kulalamikia siasa za kijeshi na mauaji yanayofanywa na utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya watoto wachanga katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, bado yanaendelea.

Kuhusiana na jambo hilo, umati mkubwa ya wananchi wa Uturuki ulikusanyika mbele ya ubalozi mdogo wa Israel mjini Istanbul, na kwa mara nyingine tena kuonyesha kuchukizwa kwao na siasa za kibaguzi za Israel dhidi ya Waislamu wa Palestina. Waandamanaji hao walichoma moto jengo la ubalozi huo ikiwa ni kujibu jinai za Israel huko Rafah. "Mahmoud Kar", msemaji wa waandamanaji hao, alisema: "Mashambulizi ya Israeli dhidi ya watu wasiokuwa na ulinzi wa Gaza yamekuwa yakiendelea mtawalia  kwa miezi 8. Nchi zote za dunia zinapaswa kuwa na umoja na kushikamana ili kuzuia jinai zaidi zinazofanywa na Israel dhidi ya Waislamu wa Palestina huko Gaza."

Maandamano ya Waturuki mbele ya ubalozi mdogo wa Israel  yalifuatana na maandamano mengine dhidi ya Israel mjini Istanbul. Kundi jingine la wakazi wa Istanbul katika eneo la "Sarachkhaneh" kitongoji cha Fatih pia limefanya maandamano dhidi ya Israel. Huku wakiwa wamebeba bendera za Uturuki na Palestina, waandamanaji hao waliwasomea dua mashahidi waliouawa katika mashambulizi ya Israel huko Palestina. Kundi jingine pia lilikusanyika mbele ya ubalozi mdogo wa Marekani katika kitongoji cha "Sarir" kupinga sera na misaada ya nchi hiyo kwa utawala katili wa Israel.Kuchomwa moto ubalozi mdogo wa Israel mjini Istanbul kunaonyesha kukithiri  chuki ya mataifa ya Kiislamu dhidi ya jinai na uhalifu unaoendelezwa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza. Kwa mfano, baada ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya kambi ya wakimbizi wa Kipalestina katika mji wa Rafah, ambayo yalipelekea kuuawa shadidi Wapalestina wasiopungua 40  duru mpya ya maandamano makubwa na ya usiku ilianza mjini Istanbul. Waandamanaji hao pia walizitaka jumuiya za kimataifa kusitisha mashambulizi ya Israel dhidi ya raia wa Palestina. Umati mwingine pia ulikusanyika karibu na ubalozi mdogo wa Marekani ukiwa na mabango yaliyoandikwa "Free  Palestine". Waandamanaji hao walikuwa wakitoa nara za "Mauti  kwa Israeli na mshirika wake Marekani".  

Fakhruddin Alton, mwanasiasa wa Uturuki anasema, utawala ghasibu wa Israel unapaswa kushtakiwa kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu. Israel ina kiu kubwa ya damu na haitosheki kwa machozi ya watu madhulumu wa Palestina. Huko Tel Aviv, kuna utawala katili ambao unatekeleza mauaji ya halaiki mbele ya macho ya walimwengu."Huku akibainisha kuwa jumuiya ya kimataifa haikuweza kuupatia ufumbuzi wa kutosha mgogoro wa Ukanda wa Gaza, mtaalamu huyo wa Uturuki amekosoa vikali siasa za kinyama na kutozingatiwa ubinadamu za utawala wa Israel na kulitaja jambo hilo kuwa ni aibu, la kutisha na  kuchukiza sana." 

Katika hali hiyo, si tu kwamba Marekani na waitifaki wake wameshindwa kuwazuia viongozi katili na wenye kiu cha damu wa utawala wa kibaguzi wa Israel kusimamisha mauaji ya raia katika mji wa Rafah, bali pia wanawapa silaha za kuendeleza mauaji kadiri inavyowezekana, na kwa hakika ni washirika katika jinai za Israel. Hali hiyo isiyo ya kawaida katika dunia ya leo inaonesha kuwa Marekani, ambayo inadai kuwa ni mtetezi wa haki za binadamu, imeshindwa kutatua matatizo ya jamii za kimataifa. Viongozi wa Marekani wanataka kujipatia manufaa zaidi kutoka kwa waliwengu na wanaendeleza himaya yao kwa utawala katili wa Israel, kwa dhana ya kujipatia maslahi zaidi. Hii ni katika hali ambayo faili la utawala huo ghasibu wa Israel litafungwa hivi karibuni kutokana jinai zake kubwa dhidi ya binadamu, na utawala huo wa kibaguzi utafutwa kabisa duniani.

342/