Main Title

source : Parstoday
Jumatano

29 Mei 2024

20:54:48
1462130

Tal al Sultan; Hospitali pekee inayofanya kazi katika mji wa Rafah

Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuwa ni hospitali moja tu ambayo imebaki inayotoa huduma katika mji wa Rafah kufuatia mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni.

Wizara ya Afya ya Gaza jana ilitangaza kuwa, ni hospitali moja tu iliyosalia kwa ajili ya matibabu katika mji wa Rafah baada ya utawala wa kizayuni kuzishambulia kwa makusudi hospitali na vituo vingi vya afya katika mji huo. Hiyo ni hospitali ya Tal al Sultan inayohusika na masual aya uzazi na magonjwa ya wanawake.  

Hospitali ya Abu Yusuf al Najjar, zahanati kuu ya Abu Walid, hospitali ya Rafah, hospitali ya utaalamu bingwa wa tiba ya al Kuwait, hospitali ya Indonesia na zahanati ya Tal al Sultan hazifanyi kazi hivi sasa ikiwa ni natija ya kuendelea mashambulizi na mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel katika mji wa Rafah. Katika muktadha huo mama wa Kipalestina aliyefiwa na kaka yake na watoto wake katika shambulio la kikatili la utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah aliinua kichwa chake mbinguni na kusema: Mwenyezi Mungu warudishie yale yote ambayo Marekani na Israel wametufanyia.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa taarifa katika radiamali yake kwa jinai za utawala wa Kizayuni zinazoongezeka kila uchao katika mji wa Rafah kwamba: Dunia inapasa kuwajibika kisheria na kimaadili mkabala na mauaji mapya na kushtadi mashambulizi ya utawala wa Kizayuni unaoikalia Quds tukufu kwa mabavu dhidi ya mahema ambayo ni makazi ya wakimbizi wa Kipalestina magharibi mwa mji wa Rafah. 


342/