Main Title

source : Parstoday
Jumatano

29 Mei 2024

20:55:40
1462132

Kiongozi wa kidini wa Iraq ataka ubalozi wa Marekani ufungwe kufuatia shambulio la Israel Rafah

Moqtada Sadr, Kiongozi wa kidini wa Iraq mwenye ushawishi amerudia wito wake wa kutaka ubalozi wa Marekani mjini Baghdad ufungwe baada ya shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuwaua makumi ya raia wa Palestina katika eneo lililodaiwa kuwa na usalama katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza.

Mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa Jumapili usiku na jeshi la Kizayuni yaliwaua shahidi Wapalestina wasiopungua 45 katika kambi ya watu waliolazimika kuhama makazi yao huko Rafah, mji wa kusini wa Gaza ambako Israel ilianzisha mashambulizi mapema mwezi huu. Sadr amelaani shambulio hilo la utawala katili wa Israel na uungaji mkono wa "kuaibisha" wa Marekani kwa mauaji ya kimbari ambayo amesema yangalia yanaendelea kufanywa huko Ghaza.Katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa kijamii wa X, Kiongozi huyo wa kidini wa Iraq amesema: "ninasisitiza juu ya takwa langu la kumfukuza balozi wa Marekani na kufunga ubalozi kwa njia za kidiplomasia bila umwagaji damu".

 Sadr ameongezea kwa kusema, hicho kitakuwa kizuizi athirifu zaidi kuliko matumizi ya nguvu na kitamaanisha kwamba maafisa wa Marekani hawatakuwa na kisingizio cha kuvuruga uthabiti ndani ya Iraq.../

342/