Main Title

source : Parstoday
Jumatano

29 Mei 2024

20:56:06
1462133

Waziri wa Uchumi: Iran imefikia hatua ya ukuaji endelevu wa kiuchumi

Waziri wa Masuala ya Uchumi na Fedha wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran imefikia hatua ya ukuaji thabiti wa uchumi.

Seyed Ehsan Khandozi ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kubainisha kuwa kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia, kiwango cha umaskini nchini Iran kimepungua kwa asilimia 7.4 na kufikia asilimia 21.7 kutoka asilimia 29.3  Waziri wa Uchumi na Fedha wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni za mashirika ya kimataifa na Benki ya Dunia, ukuaji wa uchumi wa Iran umefikia hatua thabiti; na msamiati wa kuwa na uimara umetumika kubainisha ukuaji wa uchumi wa Iran.Khandozi ameendelea kueleza kwamba: Benki ya Dunia na taasisi za kimataifa haziwaangalii watu na serikali ya Iran kwa jicho la huruma, lakini kasi ya ukuaji wa uchumi imekuwa kubwa kwa namna ambayo haikuwezekana kuipuuza na akaongeza kuwa ukuaji wa uchumi wa mwaka huu na mwaka ujao uliotabiriwa na Benki ya Dunia ni mkubwa zaidi ya mwaka uliopita na mwelekeo uliotabiriwa ni wa kuendelea kupanda uchumi wa Iran.

 Waziri wa Uchumi wa Iran amesisitizia kutokuwa na tija uafriti wa Marekani dhidi ya Tehran na akasema: "uendeshaji uchumi wa nchi haukuchelewesha kwa sababu ya mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA; na mageuzi makubwa yamefanywa katika uga wa kujenga mawasiliano na majirani na nchi washirikia; tumejenga mawasiliano na Saudi Arabia, tumekuwa mwanachama wa BRICS, fedha za Iran zilizokuwa zimezuiliwa nchini Korea Kusini ambazo hazikuweza kupatikana hata katika kipindi cha JCPOA zimerejeshwa na tumetoa jibu kali na la kihistoria pia kwa utawala wa Kizayuni". Halikadhalika, Khandoozi ameongeza kuwa mfumuko wa bei ulipungua hadi 37% mwishoni mwa mwezi uliopita na mfumuko wa bei wa hatua kwa hatua umefikia 31%.../

342/