Main Title

source : Parstoday
Jumatano

29 Mei 2024

21:01:52
1462141

Sayyid Hassan Nasrullah asema utawala wa Israel wa 'Kinazi' hautadumu katika eneo

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuhusu mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza kwamba, jinai hiyo ya kutisha uliyofanya utawala huo ghasibu inapasa iwaamshe na kuwatoa kwenye usingizi wa mghafala watu waliojisahau duniani na walioshindwa kuwa na msimamo.

Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kwamba watu waliojisahau na wasio na msimamo duniani wanapaswa kuzinduka kutoka kwenye usingizi wa mghafala baada ya kuona jinai za kutisha za utawala ghasibu wa Kizayuni huko Rafah na akaongezea kwa kusema, utawala huo hauna hisia za utu au misingi ya kimaadili na ni mbaya zaidi kuliko Wanazi.Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameeleza bayana kuwa jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Ghaza zinadhihirisha unyama, uhaini na woga ulionao utawala huo haramu.Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa jinai za kutisha ulizofanya utawala wa Kizayuni Rafah zitaongeza kasi ya kusambaratika utawala huo ghasibu na kwamba utawala huo wa Kinazi hautadumu kwa namna yoyote katika eneo hili.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, jamii ya kimataifa haina uwezo na dhaifu katika kukabiliana na jinai za utawala bandia wa Kizayuni na inatosheka tu na kutoa taarifa za kulaani na kuonyesha kwamba inatiwa wasiwasi na yanayojiri.

Wapalestina wanaokaribia 50 wakiwemo wanawake na watoto waliuawa shahidi na 249 walijeruhiwa katika shambulio la kinyama la makombora lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel usiku wa manane wa Jumapili iliyopita lililolenga kambi ya wakimbizi katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Ghaza.Kulingana na Wizara ya Afya ya Palestina, karibu nusu ya waliouawa shahidi katika shambulio hilo walikuwa wanawake, watoto na wazee.../

342/