Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

7 Juni 2024

15:08:49
1463967

HAMAS yatoa vipigo vingine vikali kwa wanajeshi vamizi wa Israel

Brigedi za Shahid Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kuwa zimeendelea kuviwinda na kuvitwanga kwa makombora vifaru vya utawala wa Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza.

Katika ripoti yake ya jana Alkhamisi, tawi hilo la kijeshi la HAMAS limetangaza kuwa, limevitwanga na kuviteketeza vifaru vitatu vya Israel aina ya Merkava mashariki mwa mji wa Dayr al Balah katikati mwa Ukanda wa Ghaza, kwa kutumia roketi aina ya Yasin 105.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanamapambano wa HAMAS walitega mabomu kwenye handaki moja katika eneo la Tel al Za'rab magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kuangamiza wanajeshi watano wa Israel walioingia kwenye mtego huo.

Vilevile Brigedi hizo za Izzuddin Qassam zimeendelea kuvipiga kwa makombora vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko karibu na Ukanda wa Ghaza kwa kutumia maroketi na makombora tofauti. Mashambulizi yote hayo ni katika kujibu jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina hasa wa Ukanda wa Ghaza. Tangu tarehe 7 Oktoba 2023 hadi hivi sasa utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya jinai za kutisha ambazo hazijawahi kutokea dhidi ya wanawake, watoto wadogo na raia wa kawaida wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza mbele ya kimya cha makusudi cha jamii ya kimataifa na uungaji mkono wa pande zote wa madola ya kibeberu hasa Marekani kwa jinai hizo za Wazayuni.

342/