Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

7 Juni 2024

15:13:09
1463974

Waislamu India wapata ahueni kidogo baada ya chama cha Modi kudhoofika

Matokeo ya uchaguzi mkuu wa India yanaonyesha kuwa muungano wa Waziri Mkuu Narendra Modi umepata viti vichache sana kuliko ilivyotarajiwa.

Wataalamu wanasema kupata nguvu vyama vya upinzani  kutaleta kiwango fulani cha faraja kwa Waislamu nchini India, ambao wamekabiliwa na miaka kadhaa ya ubaguzi uliokithiri chini ya serikali ya Modi yenye misimamo mikali ya utaifa wa Kihindu wa kibaniani ujulikanao kama Hinduvata

Akizungumza na Middle East Monitor, P. K. Niaz, mwandishi wa habari mwandamizi aliyeko Qatar, amesema wakati Narendra Modi na washirika wake wa utaifa wa Kihindu wamesalia na mamlaka katika uchaguzi mkuu wa India, mafanikio makubwa ya vyama vya upinzani yatatoa faraja kwa kiwango fulani kwa Waislamu walio wachache nchini humo ambao wamekabiliwa na miongo kadhaa ya ubaguzi na ukandamizaji wa Wahindu wenye misimamo mikali.

Matokeo rasmi ya yaliyochapishwa wiki hii Tume ya Uchaguzi ya India yalithibitisha kuwa muungano wa Modi wa National Democratic Alliance (NDA), ambao unajumuisha chama chake cha mrengo wa kulia cha Hindutva, Bharatiya Janata Party (BJP), ulishinda viti 294, ikiwa ni zaidi ya viti 272 vinavyohitajika ili kupata uongozi wa bunge, lakini ni chini ya ilivyotarajiwa. Kwa mara ya kwanza tangu BJP ilipoingia madarakani mwaka wa 2014, haikupata wingi wa kura peke yake, ikishinda viti 240, chini ya rekodi 303 iliyoshinda katika uchaguzi wa 2019. Muungano wa upinzani unaoongozwa na Chama cha Congress unaojulikana kama INDIA, ambao unaungwa mkono kikamilifu na Waislamu, ulipata viti 223.

Matokeo ya hayo ya uchaguzi yanaonyesha kuwa magenge Hindutva ya Modi, ambayo huwashambulia Waislamu, hayawezi tena kuwa na mkono huru katika kutekeleza ajenda yao dhidi ya Uislamu.

342/