Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

8 Juni 2024

18:24:31
1464256

Iran: Kususia bidhaa za utawala wa Kizayuni ni hatua nyepesi zaidi lakini ndio athirifu zaidi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Iran amesema, kuzisusia bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel ndio hatua madhubuti na athirifu zaidi ya kukabiliana na ulegevu wa kutochukua hatua unaoonyeshwa na serikali mbalimbali duniani na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Nasser Kanani, ameeleza hayo katika andiko aliloweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X akizungumzia siku 245 za mashambulio ya mtawalia, ya pande zote na ya kinyama yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina waliowekewa mzingiro wa Ukanda wa Ghaza na mauaji ya kutia uchungu ya wanawake na watoto wa eneo hilo na akasema: "kutokana na kutochukua hatua serikali na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa za kusimamisha jinai za kivita za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, wajibu wa mataifa na asasi za kiraia wa kulisaidia taifa madhulumu la Palestina unaongezeka zaidi". Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amebainisha kuwa: kususia bidhaa na makampuni ya Kizayuni ni jambo rahisi zaidi lakini lina taathira kubwa sana.Idara ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetangaza katika taarifa kwamba tangu vilipoanza vita, watoto 17,000 wa Kipalestina wamepoteza wazazi wote wawili au mmoja wa wazazi wao.

 Imeelezwa katika taarifa hiyo kuwa, watoto wengine 3,500 wako hatarini kufariki dunia huko Ghaza kutokana na utapiamlo na uhaba wa chakula uliosababishwa na vita. Ripoti hiyo imetolewa huku Umoja wa Mataifa ukijiandaa kuuweka utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye orodha nyeusi kwa kuhusika na mauaji ya watoto wa Kipalestina. Mashambulio ya kinyama yanayokinzana na vipimo vya kibinadamu na sheria za kimataifa ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza yameibua malalamiko makubwa ya maoni ya umma, taasisi za kiraia na mashirika ya kimataifa, mbali na Umoja wa Mataifa uliotoa mjibizo mkali, na kupelekea baadhi ya mashirika na taasisi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa wenyewe kutoa wito kwa Katibu Mkuu wake achukue hatua dhidi ya Israel.../

342/