Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

8 Juni 2024

18:26:10
1464259

Putin: Russia itashinda, mzozo wa Ukraine utamalizika kwa kuridhiwa matakwa yake

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, mzozo wa Ukraine utamalizika kwa kukubaliwa matakwa na masharti ya nchi yake.

Putin ameeleza hayo alipoulizwa kuhusu mzozo wa Ukraine na akafafanua kwa kusema: "mazungumzo yote yanatokana na kushindwa kijeshi, au ushindi wa kijeshi. Bila shaka tutashinda”. Akizungumza kwenye jopo la maswali na majibu lililofanyika pembeni ya Jukwaa la Kiuchumi la Kimataifa la St. Petersburg (SPIEF), Rais wa Russia amesema, uongozi wa Kiev hauna uhalali wa kisheria na kwamba nchi za Magharibi haziwezi kuaminiwa.Putin amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, Moscow iko tayari kwa mazungumzo, lakini inahitaji kuwa na uwezo wa kuwaamini watu wa upande mwingine na kupewa masharti ambayo ni kwa maslahi yake; na akaongezea kwa kusema: mazungumzo ya amani hayawezi kutegemea "mawazo ya kinjozi".

Rais wa Russia ameihutubu pia hadhira ya SPIEF ya kwamba Volodymyr Zelenskyy hawezi kuhesabiwa kuwa rais halali wa Ukraine kwa sababu muhula wake ulishamalizika kisheria tangu mwezi uliopita. Amesema, Katiba ya Ukraine iko wazi kuhusu kuongezwa muda wa mamlaka ya bunge katika hali ya dharura, lakini haisemi chochote kuhusu mihula ya urais. Kwa hivyo madai ya Zelenskyy ya kubaki madarakani hayana uhalali.

Putin ameongeza kuwa Russia italazimika kutafuta mtu mwingine wa kuamiliana naye.../

342/