Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

8 Juni 2024

18:26:51
1464260

Wanaharakati wa Kiyahudi waitaka Ujerumani iache kuipelekea silaha Israel

Wanaharakati wa Kiyahudi wameitaka serikali ya Ujerumani iache kuupatia silaha utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wanaharakati hao wametoa mwito wao huo katika maandamano mbele ya Ubalozi wa Ujerumani huko Tel Aviv na kusisitiza kwamba, serikali ya Berlin inapaswa kusitisha uuzaji wa silaha kwa utawala huo ghasibu.

Waandamanaji walioketi kwenye lango la ubalozi wa Ujerumani mjini Tel Aviv walibeba mabango yenye maandishi: “Acheni kuipa Israel silaha” na “Je, hamna umwagaji wa damu wa kutosha mikononi mwenu?” Na "kuweni upande sahihi wa historia kwa mara moja."

Waandamanaji hao pia walituma barua kwa balozi wa Ujerumani, Steffen Seibert, wakitaka utawala wa Berlin usitishe uuzaji wa silaha kwa utawala dhalimu wa Israel.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umeongeza jeshi la Israel kwenye "orodha ya aibu" ya kila mwaka ya wahalifu wanaoua watoto.Gilad Erdan, balozi wa utawala wa Israel katika Umoja wa Mataifa, alifahamishwa rasmi kuhusu uamuzi huo ambao umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, siku ya Ijumaa.

Orodha hiyo imeambatanishwa na ripoti kuhusu watoto na mizozo ya kivita ambayo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa huwasilisha kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kila mwaka.

Orodha hiyo imetangazwa wakati utawala haramu wa Israel unaendeleza vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7 mwaka jana (2023).


342/