Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo mchana wakati alipoonana na wakuu wapya na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Shahid Motahari na kusema katika sehemu moja ya miongozo yake kuhusu uchaguzi wa keshokutwa Ijumaa wa duru ya pili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa, uchaguzi huo ni muhimu sana na yeyote mwenye uchungu wa nchi, mwenye uchungu na Uislamu na anayependa ustawi na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu basi lazima atashiriki kwenye uchaguzi huo.
Aidha amemesema, wale wanaodhani kwamba kila ambaye hakushiriki katika uchaguzi uliopita anaupinga mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, ajue anakosea sana, kwani licha ya kwamba maadui wanaeneza propaganda kubwa za kuhakikisha watu hawajitokezi kwa wingi katika chaguzi za nchini Iran, lakini wameshindwa na kwamba si kila asiyeshiriki kwenye uchaguzi ni mpinzani wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.Kampeni za uchaguzi wa duru ya pili wa urais nchini Iran zilianza rasmi Jumapili yaani siku moja tu baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Juni 28. Masoud Pezeshkian na Saeed Jalili walipata idadi kubwa zaidi ya kura lakini hakuna mgombea aliyefanikiwa kupata zaidi ya nusu ya kura, hivyo uchaguzi huo uliingia kwenye duru ya pili. Zaidi ya watu milioni 24 walipiga kura katika uchaguzi wa Ijumaa iliyopita wa kuchukua nafasi ya Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, ambaye alipoteza maisha katika ajali ya helikopta Mei 19.
342/