Uchaguzi wa kesho unafanyika baada ya uchaguzi wa raundi ya kwanza Ijumaa iliyopita kutokana na kuuwa hakuna mgombea aliyepata iddai ya kura ambazo angetangazwa mshindi wa mujibu wa katiba.
Duru hiyo ya pili ya uchaguzi iliyopangwa kufanyika kesho Julai 5, itawachuanisha aliyekuwa Waziri wa Afya na mbunge wa sasa, Masoud Pezeshkian na mkuu wa zamani wa timu ya mazungumzo ya nyuklia, Saeed Jalili.
Katika matokeo ya duru ya kwanza baada ya kuhesabiwa kura zote zilizopigwa (24,535,185) kwenye uchaguzi huo wa Ijumaa iliyopita Juni 28, Pezeshkian aliibuka kidede kwa kupata kura 10,415,991 huku Jalili akiambulia kura 9,473,298.
Tayari wagombea wa kiti cha Urais leo wamekamilisha kampeni zao za uchaguzi ambapo kwa mujibu wa katiba kampeni zinapaswa kumalizika masaa 24 kabla ya kufanyika uchaguzi.
Watalamu wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa, uchaguzui wa kesho wa Rias nchini Iran unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa n ani vigumu kutabiri mshindi hasa kutokana na mchuano mkubwa ulionekana baina ya wagombea hao wawili katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo, kwenye midahalo n ahata katika uchunguzi wa maoni. Tume ya uchaguzi imetangaza kuwa, iataanza kutoa matokeo ya awami mara tu baada ya kukamilika zoezi la upigaji kura na kuanza kazi ya kuhesabu kura. Hadi kufikia Jumamosi Iran inatarajiwa kuwa itakuwa imempata Rais atakayeziba pengo la shahidi Ebrahim Raisi aliyeagha dunia katika ajali ya helikiopta Mei 19 mwaka huu akiwa na maafisa wengine akiwemo Waziri wake wa mashauri ya kigeni Hussein Amir Abdollahian.
342/