Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

4 Julai 2024

16:06:54
1469649

Kaimu Rais wa Iran: Mataifa ya dunia yachukue hatua za haraka kuhitimisha jinai za kivita za Israel

Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyataka mataifa ya dunia kuchukua hatua za haraka kuhitimisha jinai za kivita za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina hususan katika Ukanda wa Gaza.

Muhammad Mokhber amesema hayo katika hotuba yake kwenye Kikao cha Viongozi wa Jumuiya ya Shanghai huuko Astana, mji mkuu wa Kazakhstan na kubainisha kwamba, kwa bahati mbaya, katika kipindi cha miezi 9 iliyopita na kinyume na viwango vyote vya kimataifa na maadili ya binadamu, tunashuhudia wimbi kubwa la mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, mauaji ya umati ya wanawake na watoto wasio na hatia wa Gaza yanayofanywa na utawala wa Kizayuni.

Kaimu Rais wa Iran amesisitiza kuwa, tunalaani vikali kuendelea jinai za kinyama na za kupangwa zinazofanywa na utawala wa Kizayuni kwa uungaji mkono wa Marekani dhidi ya wananchi wanamuqawama na madhulumu wa Gaza.

Aidha ametaka kutumiwa fursa zilizopo baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Shanghai ili kuboresha maisha ya wananchi na wakati huo kuleta ustawi na maendeleo baina ya mataifa wanachama.

 

Iran inashiriki kama mwanachama kamili, wa kudumu na kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Shanghai unaofanyika Kazakhstan, na hiyo ni fursa muhimu sana kwa sababu viongozi wakuu wapo katika mkutano huu.

Iran ilikubaliwa kuwa mwanachama kamili katika mkutano wa 23 wa kilele wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ulioandaliwa na India na hivyo kupatikana fursa nyingi za kipekee baina ya Iran na nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

342/