Duru ya pili ya uchaguzi wa 14 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itafanyika kesho Ijumaa Julai 5. Masoud Pezeshkian na Saeed Jalili Ijumaa iliyopita waliingia duru ya pili ya uchaguzi huo wakiwa wagombea wawi waliopata kura za juu zaidi. Uchaguzi wa Rais wa Iran unafanyika karibu mwaka mmoja kabla ya muda uliopangwa baada ya kufa shahidi Sayyid Ebrahim Raisi na viongozi wengine wa serikali katika ajali ya helikopta kaskazini magharibi mwa Iran.
Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumatano alisisitiza umuhimu wa awamu hii ya uchaguzi wa rais na kusema kwamba, uchaguzi huu ni muhimu sana na kwamba kila mtu anayeunga mkono Uislamu, Jamhuri ya Kiislamu, maendeleo na ustawi wa nchi na suala la kuondoa mapungufu yaliyopo, anaweza kuonyesha uungaji mkono huo siku ya Ijumaa kwa kushiriki katika uchaguzi. Katika sehemu nyingine ya maelezo yake, Ayatullah Khamenei alisema kuwa mchakato wa uchaguzi bado haujaisha, na ameutaja ushiriki wa wananchi kuwa ndio nguzo muhimu na fahari ya utawala wa Kiislamu hapa nchini. Vilevile ameeleza matumaini yake kuwa Mwenyezi Mungu atawapa wananchi taufiki ya chaguo bora zaidi ili mtu atakayechaguliwa aweze kutimiza malengo ya utawala wa Kiislamu na taifa. Duru ya 14 ya uchaguzi wa rais wa Iran itafanyika kesho huku hali ya ndani, kieneo na kimataifa ikiongeza maradufu umuhimu na unyeti wake. Ni kwa sababu hiyo, ndiyo maana katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kislamu amekuwa akisisitiza mara kwa mara umuhimu wa kipindi hiki cha uchaguzi na ushiriki mkubwa wa tabaka mbalimbali za watu katika zoezi hilo. Ni wazi kuwa ushiriki wa watu wengi zaidi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais sambamba na kuimarisha misingi ya utawala, vilevile utazidisha imani na hali ya kujiamini ya umma. Viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hususan Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, daima wamekuwa wakitilia mkazo ushiriki mkubwa wa wananchi katika chaguzi zinazofanyika hapa nchini na kuutaja kuwa ni wajibu na haki kwa wakati mmoja. Msisitizo huu unatokana na ukweli kwamba, sifa ya "jamhuri" katika utawala wa Kiislamu inatimia kwa ushiriki wa watu. Kuhusiana na hilo, tunaweza kusema pia kwamba, ushirikiano wa wananchi na utawala wa Jamhuri ya Kiislamu mbali na kuimarisha nguvu ya mamlaka ya kitaifa, ni nguzo muhimu katika kuundwa serikali imara ili iweze kutekeleza vyema shughuli zake hususan katika nyanja za kiuchumi na kisiasa. Kwa hakika, hali ya sasa ya Iran na njama zinazofanywa na maadui za kutaka kuanzisha mpasuko kati ya wananchi na utawala wa Kislamu, vinazidisha ulazima wa kutayarishwa mazingira bora ya ushiriki mkubwa wa wananchi katika uchaguzi wa rais wa kesho, ili mbali na kuzima njama za maadui, kwa mara nyingine tena waonyeshe irada na azma ya taifa ya kulinda thamani na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu.
342/