kabla ya kuondoka kuelekea Kazakhstan kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai huko Astana, "Mohammed Mokhbir" amesisitiza kuwa: "Moja ya mafanikio makubwa ya marhum Rais Raisi aliyekufa shahidi katika ajali ya helikopta tarehe 19 Mei, katika upande wa kidiplomasia ni uanachama wa Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, BRICS na Biashara Huria ya Eurasia.
Amesema, kwa baraka za mafanikio hayo, leo hii wanaharakati wa masuala ya kiuchumi wa Iran wanaweza kutumia fursa nyingi na za kipekee zinazopatikana kwenye jumuiya hizo, kustawisha uchumi wa nchi yao kadiri wanavyoweza.Kaimu Rais wa Iran ameongeza kuwa: Tehran inashiriki kama mwanachama kamili, wa kudumu na kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Shanghai unaofanyika Kazakhstan, na hiyo ni fursa muhimu sana kwa sababu viongozi wakuu wapo katika mkutano huu. Amesema: Pembeni mwa mkutano huo kutafanyika vikao mbalimbali baina ya Iran na pande kadhaa kwa nyakati tofauti na miongoni mwa maudhui muhimu zitakazojadiliwa, ni mikakati ya marhum Rais Raisi ya kulipaisha taifa la Iran katika sekta za mafuta, petro kemikali na masuala ya usafiri. Iran ilikubaliwa kuwa mwanachama kamili katika mkutano wa 23 wa kilele wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ulioandaliwa na India na hivyo kupatikana fursa nyingi za kipekee baina ya Iran na nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
342/