Duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Iran imeanza mapema leo Ijumaa katika kona zote za nchi na vyombo vya habari vya kimataifa vimeuakisi kwa wingi uchaguzi huo.
Wagombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa 14 wa rais wa Iran ni Masoud Pezeshkian na Saeed Jalili.
Shirika la habari la IRNA limeripoti leo kuwa; kanali za televisheni za Al Jazeera ya Qatar, CNN ya Marekani, France 24 ya Ufaransa, BBC ya Uingereza, shirika la habari la Armenia, gazeti la Hindustan Times, India Today, vyombo vya habari vya Jamhuri ya Azerbaijan, gazeti la Uingereza la The Guardian na vyombo vingine vingi vya habari vya Asia, vya nchi za Kiarabu na vingine vya kimataifa vimeripoti kwa wingi uchaguzi huo wa Iran.Shirika la habari la Sputnik la Russia limetangaza kuwa wananchi wa Iran wamefanya duru ya pili ya uchaguzi kwa kujitokeza kwa wingi mkubwa.
Televisheni ya China Central imeandika kwenye tovuti yake ya habari kwamba wananchi wa Iran wamejitokeza kwa wingi leo Ijumaa kumchagua rais wao wa baadaye kati ya wagombea wawili, Masoud Pezeshkian na Saeed Jalili.
Shirika la Habari la Uturuki la Anadolu limeripoti habari hiyo na kusema kuwa uchaguzi huo ni wa kumchagua mtu wa kuziba nafasi ya Sayyid Ebrahim Raisi, rais wa zamani wa Iran aliyekufa shahidi katika ajali ya helikopta tarehe 19 Mei mwaka huu wa 2024.
342/