Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

6 Julai 2024

16:34:53
1470012

Jalili ampongeza Pezeshkian kwa ushindi wa kiti cha Rais wa Iran

Saeed Jalili, ametoa ujumbe akimpongeza Massoud Pezeshkian aliyechuana naye katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu baada ya mapema leo asubuhi Wizara ya Mambo ya Ndani kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika jana kote nchini.

Saeed Jalili, amesema katika ujumbe huo kwamba, jana tarehe 5 Julai, taifa kubwa la Iran, kwa mara nyingine tena, limeionyesha dunia uthabiti na uimara wa misingi ya demokrasia ya kidini na nafasi ya jamhuri kwa ushiriki mpana sambamba na ushindani mkubwa katika mazingira yenye afya na usalama.

Saeed Jalili amesema: Sasa ni juu ya kila mtu kuheshimu chaguo la wananchi na kumsaidia katika maendeleo ya nchi na kuinua juu mfumo mtakatifu wa Jamhuri ya Kiislamu.

Jalili pia amempongeza mshindani wake katika uchaguzi wa rais na kusema: "Kama ilivyokuwa huko nyuma, naona ni wajibu wangu kuisaidia katika kuondoa matatizo yaliyopo na kuifikisha nchi katika hatua inayotakikana ya maendeleo."

Amesisitiza kuwa, sasa ni wakati wa kila Muirani kutoa mchango mkubwa kwa mshikamano na umoja wa kitaifa ili kufikia malengo makubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu.

342/