Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Julai 2024

15:16:33
1470288

Kiongozi wa Mapinduzi: Shahid Raisi, ni kigezo cha uongozi kwa serikali na viongozi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametaja juhudi zisizokoma za kutatua matatizo ya watu, imani kubwa juu ya uwezo wa ndani, kuwa wazi katika kutangaza misimamo ya kidini na kimapinduzi, kutochoka, kutokata tamaa, kujitolea katika utekelezaji wa mipango mikubwa, unyenyekevu na uvumilivu na kushikamana na masuala ya kiroho, dhikri na kutawasali kuwa nii miongoni mwa sifa bora za kibinafsi, kimienendo na za kikazi za Shahid Ebrahim Raisi.

Ayatullah Ali Khamenei, ameyasema hayo mapema leo alipokutana na Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu na baraza la mawaziri na kusisitiza kuwa: Shahidi Raisi alionyesha kuwa mtu anaweza, kama rais wa nchi, kujipamba kwa sifa za kifikra, kiroho na kimatendo na kuzitekeleza kivitendo.

Katika kikao hicho, ambacho kilikuwa cha mwisho cha baraza la mawaziri la Serikali ya Awamu ya 13, Ayatullah Khamenei ameitaja serikali ya 13 kuwa ni serikali ya "kazi, matumaini na harakati" na kusema: Shahidi Ebrahim Raisi alikuwa na matumaini kuhusu mustakbali mwema, na alikuwa na maamuzi thabiti ya kufikia malengo yaliyoainishwa.

Akieleza sifa kuu za hayati Raisi, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kislamu amekutaja kuwa karibu na watu kuwa ndio sifa muhimu sana na mfano wa kuigwa kwa viongozi wote na akasema: Raisi aliwaheshimu wanachi, na alihisi hali halisi na mahitaji yao kwa kuwa baina yao. Vilevile alilipa kipaumbele suala la kutatua matatizo yao.
Ayatullah Khamenei ameitaja imani ya kina ya uwezo wa ndani ya nchi kuwa ni sifa nyingine mashuhuri ya Shahidi Raisi na akasema: Sayyid Raisi alikuwa na imani kubwa kwa uwezo wa ndani kwa ajili ya kutatua matatizo ya nchi. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amewapongeza wajumbe wa baraza la serikali kwa kushirikiana na Shahidi marehemu Ebrahim Raisi na kusisitiza kuwa, kama si ushirikiano huo kazi hizi zote zisingefanyika. Rais Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, na ujumbe walioandamana nao walikufa shahidi baada ya helikopta iliyokuwa imewabeba kuanguka katika mkoa wa kaskazini-magharibi wa Azarbaijan Mashariki Mei 19, 2024. 

342/