Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kwa mkutano wa 58 wa Muungano wa Jumuiya za Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya ulikuwa mfupi lakini una nukta kadhaa muhimu za kuzingatia.
Nukta ya kwanza ni hii kwamba, mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu juu ya Muungano wa Jumuiya za Wanafunzi wa Kiislamu ni mtazamo wa kitaasisi na wa pamoja.
Mtazamo kama hu ni mithili ya imani katika uwezo wa kitaasisi na wa pamoja wa shughuli za kisiasa na kitablighi.
Kwa msingi huo, Kiongozi Mkuu wa mapinduzi alisisitiza taathira chanya ya umoja huo katika masuala makubwa ya kikanda na kimataifa.
Nukta nyingine ilikuwa kwamba, Kiongozi Muadhamu anaamini kwamba wanafunzi wa Kiislamu ni "mtaji wa thamani" ambao kwa motisha, imani na kujiamini wanaweza kuwa na nafasi amilifu katika masuala makubwa na kama alivyosema Kiongozi Muadhamu "katika masuala muhimu na majeraha mpya na ya zamani ya ulimwengu".
Ni kwa kuzingatia hilo ndio maana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya kutumiwa uwezo wa pamoja na wa mtu binafsi wa Muungano wa Jumuiya za Wanafunzi wa Kiislamu.
Nuktta ya tatu katika ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa wanafunzi wa Kiislamu ulikuwa ni kueleza utendaji wa ulimwengu wa Magharibi katika masuala muhimu ya dunia.
Kwa mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kuwa, suala la hivi karibuni kabisa na la muhimu zaidi duniani ni maafa yasiyo na kifani katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi, maafa ya Ukanda wa Gaza yalikuwa ni kushindwa kimaadili, kisiasa na kijamii kwa nchi za Magharibi, wanasiasa wa Magharibi na ustaarabu wa Magharibi.
Tafsiri hii ya kiongozi wa mapinduzi inatokana na jinai za kinyama za Wazayuni wanazozifanya huko Ukanda wa Gaza kila siku wanazifanya kwa njia ya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza, na hasa makumi ya maelfu ya wanawake na watoto wa Gaza ambao wameuawa shahidi na kujeruhiwa, na kuzuia kuingia misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza na kusababisha njaa kali kwa watu hao.
Viongozi wa Magharibi wametangaza wazi na rasmi kwamba, wameunga mkono jinai hizo ambapo sambamba na kuisaidia Israel kisilaha na kimaada, wamezuia kuchukuliwa hatua yoyote ile na asasi za kimataifa kwa ajili ya kusitisha jinai hizo za Wazayuni.Nukta ya nne katika ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Muungano wa Jumuiya za Wanafunzi wa Kiislamu ulikuwa ni kukosoa demokrasia ya kiliberali. Demokrasia ya kiliberali ya Magharibi inadai kuunga mkono haki za binadamu, hasa uhuru wa kusema na haki, lakini ushahidi unaonyesha kwamba, ni bwabwaja na maneno matupu tu, na kivitendo, Wamagharibi wana mtazamo wa kuchagua na wa kibaguzi katika utekelezaji wake. Tofauti ya kimtazamo kati ya mgogoro wa Ukraine na Ukanda wa Gaza pia unathibitisha mtazamo huu wa kuchagua mambo katika demokrasia ya kiliberali ya Magharibi.
Katika suala hili, Kiongozi Muadhamu amesisitiza juu ya "kutokuwa na uwezo demokrasia ya kiliberali na wadai wake wa kuleta uhuru wa kujieleza na kughafilika kwao pakubwa na suala la uadilifu wa kiuchumi na kijamii". Jambo la mwisho katika ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kuashiria kwake, maandamano na malalamiko ya wanafunzi huko Marekani na Ulaya, ambayo pia alitaja kuwa moja ya masuala muhimu zaidi katika ulimwengu wa leo.
Kiongozi wa mapinduzi ya Kiislamu alitaja tukio hilo kama "cheche iliyofifia, lakini yenye matumaini". Inaonekana kuwa, makusudio ya Kiongozi Muadhamu ya ibara hii ni matumaini ya kuboresha suala kutetea uhuru wa kusema, uadilifu wa kiuchumi na kijamii katika nchi za Magharibi.