Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Julai 2024

15:17:47
1470290

Balozi wa Iran UN awasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama kufuatia madai yasiyo na msingi ya Arab League

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amewasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu madai ya uwongo yaliyotolewa na Jumuia ya Nchi za Kiarabu kuhusu Iran.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, katika barua yake kwa Baraza la Usalama la UN, Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani vikali na kukadhibisha tuhuma za uwongo na zisizo na msingi dhidi ya mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Iran zilizobainishwa katika kifungu cha 11 cha taarifa ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

Balozi Iravani amezitaja tuhuma hizo dhidi ya Iran kuwa ni uingiliaji wa wazi na usio wa kiadilifu katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Barua hiyo ya Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, taarifa iliyotolewa na nchi za Kiarabu dhidi ya Iran si tu kuwa ni kinyume na mwenendo wa ujirani mwema, bali inakiuka wa wazi wa kanuni za kimsingi za sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa, hasa kanuni kuhusu haki ya mamlaka ya kujitawala nchi na kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine. 

Barua ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imeendelea kubainisha kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena inasisistiza kuhusu mamlaka yake isiyoweza kukanushwa kuhusu kumiliki kwake visiwa vya Iran vya Musa, Tomb Kubwa na Tomb Ndogo katika Ghuba ya Uajemi. 

342/