Main Title

source : Parstoday
Jumapili

7 Julai 2024

15:18:15
1470291

EU: Tuko tayari kuboresha ushirikiano na Iran

Msemaji wa Umoja wa Ulaya anayehusika na sera ya mambo ya nje na usalama amempongeza Rais mteule wa Iran na kusema umoja huo uko tayari kustawisha ushirikiano wa pande mbili na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Nabila Massrali ameandika katika mtandao wa X kwamba: Umoja wa Ulaya uko tayari kushirikiana na serikali mpya ya Iran kwa mujibu wa sera na mahusiano ya pande mbili. Viongozi wengi wa ngazi ya juu wa Magharibi mwa Asia na pia katika pembe mbalimbali duniani wametuma salamu za pongezi kwa Rais mteule wa Iran. 

Massoud Pezeshkian amechaguliwa kuwa Rais wa Tisa wa Iran baada ya kuibuka na ushindi wa kura milioni 16 na 384,403 kati ya zaidi kura milioni 30 zilizopigwa. 

342/