Katika kikao hicho, Mokhber sambamba na kutoa shukurani zake kwa salamu za rambirambi na mshikamano wa serikali ya China na wananchi wa Iran kutokana na kumpoteza shahidi Rais zamani wa Iran, Sayyid Ebrahim Raisi ambaye aliaga dunia Mei 19 mwaka huu katika ajali ya helikopta na wenzake akiwa pamoja na maafisa wengine akiwemo Hussein Amir Abdollahian aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya Kiigeni wa Iran.
Katika kipindii cha uongozi wa Ebrahim Raisi, uhusiano wa Beijing na Tehran ulipiga hatua kubwa na hivi sasa inaonekana kuna azma thabiti ya pande mbili kuendeleza mkondo huu ili kuhakikisha kwamba, unastawi zaidi kuliko hapo awali.
Kwa msingi huo, Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisisitiza kuwa, azma ya viongozi wa Iran na China ya kuendeleza na kupanua ushirikiano wa pande mbili katika nyanja za kiuchumi, kibiashara na nishati ni kubwa.
Uhusiano kati ya Tehran na Beijing ulichukua hatua kubwa katika kipindi cha shahidi Rais wa zamani wa Iran, Sayyid Ebrahim Raisi, na sasa, kwa azma ya pande zote mbili, uhusiano huu unastawi zaidi kuliko hapo awali.
Ali Jamali, mtaalamu wa masuala ya kisiasa anasema hivi:
"Mahusiano kati ya Iran na China yana uungwaji mkono wa kihistoria, na hadi sasa, licha ya njama, hakujatokea dosari katika uhusiano huu. Iran na China ni nchi mbili muhimu na hakuna shaka kuwa serikali mpya ya Iran pia itaendeleza uhusiano na Beijing.
Kwa hiyo basi Rais Xi Jinping wa China alipokutana na Mokhber, kwa mara nyingine tena alitoa salamu za rambirambi kwa kufa shahidi Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wenzake, na kumtaka afikishe salamu zake kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Rais Xi Jinping wa China, alieeleza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni wa kistratijia na akafafanua kuwa, siasa za China za kupanua uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haziathiriwi na mambo ya nje.
Hali kadhalika hii ina maana kwamba Tehran na Beijing zitaendeleza kupanua wigo wake na uhusiano wao katika nyanja zote bila kuathiriwa na nguvu nyingine kama vile Magharibi, na katika suala hili, walitia saini makubaliano ya kimkakati ya miaka 25.
Kwa mujibu wa Xi Jinping, China inachokitaka ni kupanuliwa na kuimarishwa uhusiano na taifa la Iran, na katika mwelekeo huu, uhusiano kati ya pande mbili unapswa kuwekewa malengo.
Kwa vyovyote vile, Iran na China zina uwezo mkubwa wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na kupanua wigo wao. Pamoja na hayo, kiwango cha mabadilishano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili si katika kiwango kinachotakiwa, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatarajia China itaongeza uwekezaji vitega uchumi nchini Iran.
Aidha Iran inataraji kuiona China ikifungua milango na kuandaa mazingira zaidi ya masoko yake kkwa ajili ya bidhaa za Iran na kuweka mikakati kwa viwanda vyake kuuza bidhaa nje na kufungua uwekezaji nchini Iran.
Bila shaka, Iran na China zina masoko yanayovutia, na kutambua uwezo huu kunaweza kusaidia kuendeleza ushirikiano zaidi.
Hali kadhalika msimamo huo wa kimkakati wa Iran katika Asia Magharibi na uwezo wake wa nishati umezifanya jumuiya za kieneo kama vile Shanghai na BRICS kuichukulia Iran kama mshirika wao wa kuaminika wa kikanda.
Kwa vyovyote vile, Iran na China zina uwezo mkubwa wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na kupanua wigo wao bila shaka, kiasi cha mabadilishano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili si katika kiwango kinachotakiwa, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatarajia China itaongeza vitega uchumi vyake nchini Iran. Na katika kutenga zaidi masoko yake kwa viwanda vya kuuza nje na kufungua uwekezaji nchini Iran. Bila shaka, Iran na China zina soko zinazovutia, na kutambua uwezo huu kunaweza kusaidia kuendeleza ushirikiano zaidi. Hali kadhalika msimamo huo wa kimkakati wa Iran katika Asia Magharibi na uwezo wake wa nishati umeyafanya mashirika ya nje ya kanda kama vile Shanghai na BRICS kuichukulia Iran kama mshirika wao wa kuaminika wa kikanda.342/