Main Title

source : ABNA
Jumatatu

8 Julai 2024

21:01:39
1470578

Majibu kwa baadhi ya Shubhati kuhusiana na tukio la Karbala (1)

Kwa nini Imam Hussein (a.s) alikwenda Karbala hali ya kuwa alijua kwamba atauawa kishahidi ikiwa ataelekea Karbala?

Imam (a.s) alijua kwamba ikiwa ataelekea Karbala, atauawa kishahidi. Ndiyo, alijua. Lakini hili sio jambo pekee ambalo Imam alilijua. Imam alijua uhakika wa mambo mengine pia.

Shirika la habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Majibu mengi yametolewa kuhusiana na swali hili. Kwa mfano: Katika kujibu swali hili, ilmu ya Imam imefanyiwa utafiti. Lakini sisi tunataka kulijibu swali hili kwa njia nyingine.

Imam (a.s) alijua kwamba ikiwa ataelekea Karbala, atauawa kishahidi. Ndiyo, alijua. Lakini hili sio jambo pekee ambalo Imam alilijua. Imam alijua uhakika wa mambo mengine pia.

Imam (a.s) alijua kwamba kwenda Karbala ilikuwa ni matakwa na irada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Imam (a.s) alijua kwamba ikiwa hatakwenda Karbala na kusimama kidete dhidi ya dhulma, basi kwa hakika hakuna kitakachobakia kwenye Uislamu. Na ndio maana Imamu Hussein (a.s), akasema alipokuwa njiani kuelekea Karbala:

«.إنّي لا أرى المَوتَ إلاّ سَعادَةً، و لا الحَياةَ معَ الظالِمينَ إلاّ بَرَما» 

"Hakika mimi sioni mauti ila ni furaha, na sioni maisha pamoja na madhalimu ila ni mateso na dhiki." [Tuhaful oqul, 245]

Kutokana na hilo, ndio maana Imam aliamua kwenda Karbala ili kukabiliana na dhulma. Imam alikwenda Karbala ili kuwaamsha watu waliolala na kuwafahamisha kuhusu ufisadi uliofanywa na Yazid na watu wake.

Kinachoweza kuthibitisha jibu letu ni tukio la "Harrah". Ni tukio lililotokea miaka mitatu baada ya tukio la Karbala. Tukio ambalo watu wa Madina walifahamu bayana kuhusu ufisadi wa Yazid na wakaamua kusimama kidete dhidi ya Yazid.

Tafadhali chunguza na fanya utafiti juu ya tukio la "Harrah" ili ukweli wa harakati ya Imam Hussein (a.s) kuelekea Karbala udhihirike kwako zaidi.

ABNA