Main Title

source : ABNA
Jumanne

9 Julai 2024

09:14:19
1470681

Ujumbe wa Rais Mteule wa Iran ulioelekezwa kwa Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon / Uungaji mkono kwa upinzani utaendelea kwa nguvu zotee

Katika ujumbe wake wa kumshukuru Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon, rais mteule alisisitiza akisema: "Uungaji mkono kwa upinzani utaendelea kwa nguvu zote."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Rais mteule katika ujumbe alioutuma kwa Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon, akisisitiza kwamba uungaji mkono kwa Muqawamah utaendelea kwa nguvu zote, alisema: "Harakati za upinzani hazitaweza kuruhusu sera za jinai za utawala haramu wa Kizayuni ziendelee." 

 Andiko kamili la ujumbe wa Massoud Pezeshkiani ni kama ifuatavyo: 

 Mpendwa Bwana Sayyid Hassan Nasrallah Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon Nikitanguliza salamu na shukrani nyingi, nimepokea ujumbe wako muhimu na mzuri kufuatia kuchaguliwa kwangu kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

 Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikiunga mkono Muqawamah wa Wananchi wa eneo hili dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni. Uungaji mkono wa Muqawamah unatokana na siasa za kimsingi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, itikadi za Imam Ruhullah (r.a) na miongozo ya Kiongozi Muadhamu (Sayyid Ali Khamenei -M.A-) itaendelea kwa nguvu. 

 Nina imani kwamba harakati za Muqawamah katika eneo hazitauruhusu utawala huu kuendelea na siasa zake za kuchochea vita na jinai dhidi ya Wananchi Madhulumu wa Palestina na mataifa mengine ya eneo hili. 

Ninashukuru kwa dua yenu ya dhati kwa ajili yangu na ninamuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili yenu akuzidishieni hadhi na heshima zaidi, ustawi na maendeleo kwa watu wa Lebanon, na nusra ya Mwenyezi Mungu iwe kwa Mashujaa Mujahidina wa Muqawamah. 

 Masoud Pezeshkian

Rais mteule