Main Title

source : ABNA
Jumanne

9 Julai 2024

09:25:38
1470684

Kushushwa kwa bendera ya maombolezo ya Imam Hussein huko "Herat" kulikofanywa na vikosi vya Taliban / Waombolezaji 2 wa Imam Hussein (a.s) walikamatwa Magharibi mwa Afghanistan

Waombolezaji wawili wa Imam Hussein (a.s) walizuiliwa na kukamatwa na vikosi vya Taliban katika Mkoa wa "Herat" kutokana na kusimika kwao Bendera ya Maombolezo ya Hussein(a.s).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Vikosi vya Taliban viliivuta na kuishusha chini na kuichana Bendera ya Maombolezo ya Imam Hussein (a.s) Usiku wa kwanza wa Muharram katika eneo la mji wenye wakazi wengi wa Shia liitwalo "Jibrail" katika mji wa "Herat". 

 Vikosi vya Taliban pia viliwakamata wafanyabiashara wawili waliokwenda katika Ofisi ya Baraza la Ulamaa wa Shia huko "Herat" kwa sababu ya kuchanwa kwa Bendera hiyo ya Maombolezo. 

 Kulingana na Habari iliyopokelewa na Shirika la Habari la ABNA, maajenti wa kile kinachoitwa Utawala wa Taliban katika kitongoji hiki cha Mashia cha "Herat" wamepiga marufuku wachuuzi kuuza Bendera na nguo maalum za Mwezi wa Muharram. 

 Mwaka jana, wakati wa Mwezi wa Muharram, vikosi vya Taliban vilifanya kitendo kama hicho katika miji ya "Kabul" na "Ghazni", ambacho kilisababisha hasira ya Mashia nchini Afghanistan. 

 Hapo awali, katika taarifa yao kwa mnasaba wa Muharram, Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Afghanistan liliwataka Taliban kuzuia vikosi vyake kujihusisha na tabia ya kuamsha hisia za kiitikadi.