Main Title

source : Parstoday
Jumanne

9 Julai 2024

16:46:25
1470804

Pezeshkian: Kuunga mkono muqawama ni katika sera kuu za Iran

Rais mteule wa Iran amesema serikali yake ijayo itafanya kile iwezalo kuunga mkono vikosi vya muqawama katika eneo la Asia Magharibi, akisisitiza kuwa kuuunga mkono mrengo wa mapambano ni katika sera kuu za Jamhuri ya Kiislamu.

Masoud Pezeshkian amesema hayo katika ujumbe aliomtumia Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon, ambapo amemshukuru mwanachuoni huyo mwenye umri wa miaka 63 wa Lebanon kwa ujumbe wake wa kumpongeza kufuatia ushindi wake katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Iran.

Dakta Pezeshkian amesisitiza kuwa, Tehran daima imekuwa na itaendelea kuunga mkono muqawama na mapamabano ya watu wa eneo hili hasasi la Asia Magharibi mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakati huo huo, Rais mteule wa Iran amesema katika mazungumzo yake ya simu na Rais wa Russia, Vladimir Putin kuwa, anatumai uhusiano wa pande mbili wa Tehran na Moscow utaimarika zaidi katika kipindi chake cha uongozi.

Aidha Putin amemualika Dakta Pezeshkian kuhudhuria kikao kijacho cha jumuiya ya BRICS kitakachofanyika karibuni mjini Kazan nchini Russia.

Katika hatua nyingine, Rais mteule wa Iran amefanya mazungumzo ya simu na Abdul Latif Rashid, Rais wa Iraq ambapo amesema uhusiano wa kisiasa, kiuchumi, kidini, na kitamaduni baina ya mataifa haya mawili umekita mizizi na wala hauhitaji ufafanuzi, akikisisitiza kuwa anatumai ushirikiano baina ya nchi hizi katika nyuga tofauti utaimarika zaidi.

Kwa upande wake, Rais wa Iraq sambamba na kumpogeza Dakta Pezeshkian kwa kushinda uchaguzi wa 14 wa Rais wa Iran, ameutaja uhusiano wa nchi mbili kuwa imara, wa kidugu na wa jadi akieleza kuwa anatumai viongozi wa Tehran na Baghdad wataendelea kufanya juhudi za kuuboresha zaidi kwa maslahi ya mataifa haya mawili jirani.

342/