Main Title

source : Parstoday
Jumatano

10 Julai 2024

15:03:47
1471074

Pezeshkian: Iran itaendelea kuiunga mkono Syria na muqawama

Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran amesema kuwa, Tehran itaendelea kuiunga mkono Syria na muqawama kwa ujumla.

Daktari Masoud Pezeshkian amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Bashar al-Assad wa Syria na kusisitiza kwamba, Jamhuri ya Kislamu ya Iran inafuatilia suala la kuimarisha zaidi uhusiano wake na nchi rafiki ya Syria.

Aidha Rais mteule wa Iran ambaye anatarajiwa kuapishwa mwezi ujao wa Agosti amesema kuwa Tehran inafuatilia pia kuhakikiisha kuwa, makubaliano yaliyotiwa saini kati ya mataifa haya mawili yanatekelezwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Rais Bashar al-Assad wa Syria amesisitiza kwamba mahusiano kati ya Syria na Iran yanatokana na uaminifu wa pande mbili na wa kimsingi ambao chimbuko la umuhimu wake linatokana na muqawama na kusimama kidete dhidi ya sera za kujitanua katika eneo linalokabiliwa na machafuko ambalo linakodolewa macho ya tamaa na ukoloni.

Aidha jana hiyo hiyo, Rais mteule Masoud Pezeshkian alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Iraq Abdul Latif Rashid na kusema kuwa, anataraji kuwa uhusiano wa Baghdad na Tehran utaimarishwa na kupanuliwa zaidi katika kipindi kipya kwa ushirikiano wa maafisa wa ngazi za juu wa nchi mbili.

342/